Home » Biashara » MKUU wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate

MKUU wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate

06 September 2018 | Biashara
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Jensen Natal akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya kabla ya kuingia katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiangalia pasi ya kusafiria ya anayedaiwa kuwa mwekezaji wa katika shamba la Kibo and Kikafu Estate, Trevor Robert raia wa Zimbabwe ambalo anatajwa kutokuwa na uhalali wa kuwa mwekezaji wa shamba hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo walipotembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate linatajwa kuwa na mwekezaji asiye halali. 
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akimsikiliza Meneja wa Shamba la Kibo and Kikafu Estate Trevor Robert wakati akitoa maelezo ya uhalali wa kuwekeza katika shamba hilo.
Askari Polisi wakiwa wamemshikilia ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Tanzania,Jensen Natal inayotajwa kukwepa kulipa kodi ya serikali kutokana na uwekezaji katika shamba la Kibo and Kikafu Estate,Natal amekamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai.
Askari akimsindikiza Mwanasheria wa kampuni ya Tudeley Tanzania, Edward Mroso baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TudeleyTanzania,Jensen Natal na Mwanasheria wa kampuni hiyo, Edward Mroso wakiwa kwenye gari la Polisi muda mfupi baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo baada ya kutembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate.
 
 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazin.
MKUU wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa na kuwekwa rumande kwa saa 48 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate Jensen Natal pamoja na Manasheria wa kampuni hiyo Edward Mroso.
 
mbali na kukamatwa kwa Watu hao Mkuu huyo wa wilaya ameamuru kushikiliwa kwa muda kwa Pasi ya kusafiria ya anayetajwa kuwa mwekezaji wa Shamba la Kibo and Kikau Estate Trevor Robert kutokana na tuhuma za kukwepa kulipa kodi ya serikali inayokadiRiwa kuwa Zaidi ya Sh Mil 700.
Ad