Home » Makala » Fahamu faida za tikitimaji

Fahamu faida za tikitimaji

16 February 2016 | Makala

Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharibifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.

Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.

Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.

Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.

Kwa kawaida tunda hili huliwa peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake mpaka mbegu zake, ila ipo siku tutazungumzia kuhusu faida za mbegu zake, In shaa Allah.

Ad