Home » Michezo » Sharapova apoteza imani kwa wadhamini wake

Sharapova apoteza imani kwa wadhamini wake

09 March 2016 | Michezo

Saa chache baada ya kuweka wazi utumiaji wake wa dawa za kusisimua misuli, Maria Sharapova, malkia wa michezo ya biashara na mchezaji tajiri duniani kote, tayari amepotza imani kwa wadhamini wake wa kwanza Jumanne hii, na hivyo kuona mkakati wake wa masoko ukipunguka ghafla.

Kampini ilioanza kuvunja uhusiano wake na Maria Sharapova ni Nike, kisha Tag Heuer na baadaye Porsche.

Siku moja baada ya kukiri kwa mchezaji huyo wa Urusi, ambaye alikiri kutumia "kwa miaka kumi" dawa za kusisimua, hasa dawa iitwayo meldonium, dawa ambayo iliwekwa Januari 1, 2016 kwenye orodha ya bidhaa zilizopigwa marufuku, kampuni ya jezi za michezo na ile ya kutengeneza magari zimesimamisha mahusiano yao na mchezaji huyo wa Urusi.

Kampuni ya Nike imesimamisha kwa mda uhusiano wake na bingwa mara tano wa mchezo wa Tennis, Maria Sharapova, baada ya mchezaji huyo kukiri kupatikana na dawa za kusisimua misuli.

Kampuni hiyo imesema kuwa imeshangazwa na kukiri kwake kwamba alipatikana na dawa hizo katika michuano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.

Uhusiano wa Sharapova na Nike ulianza akiwa na umri wa miaka 11.

Mwaka 2010, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, aliweka kandarasi ya miaka minane na kampuni hiyo ya jezi za michezo iliokuwa na thamani ya dola milioni 70 pamoja na malipo ya nguo zake za kibinafsi.

Bi Sharapova ndiye mchezaji wa kike anayelipwa fedha nyingi baada ya kupokea dola milion 30 mwaka 2015 kutokana na ushindi pamoja na ufadhili kulingana na Forbes.

 
 
Ad