Home » Nje Ya Afrika » Bunge la nchi hiyo limeunga mkono hoja ya Waziri Mkuu Theresa May ya kufanya uchaguzi wa mapema

Bunge la nchi hiyo limeunga mkono hoja ya Waziri Mkuu Theresa May ya kufanya uchaguzi wa mapema

20 April 2017 | Nje ya Afrika

Siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May kuitisha uchaguzi wa Mapema, hatimaye Bunge la nchi hiyo limeunga mkono hoja ya Waziri Mkuu Theresa May ya kufanya uchaguzi wa mapema. Sasa uchaguzi Mkuu wa Uingereza utafanyika Juni 8 , 2017.

Theresa May, ametaka idhini kutoka kwa raia wa Uingereza katika kuendeleza mazungumzo ya mchakato wa Uingereza kuondoka Muungano wa Ulaya.

Bi Theresa May, ametaka idhini kutoka kwa raia wa Uingereza katika kuendeleza mazungumzo ya mchakato wa Uingereza kuondoka Muungano wa Ulaya.

Bunge la Uingereza limeunga mkono kwa kura 522 dhidi ya 13. Vyama vya upinzani vimeunga mkono hoja ya Waziri Mkuu.

Uchaguzi Mkuu wa Uingereza ulipangwa kufanyika mwaka wa 2020. Hata hivyo bunge linaweza kufanyia sheria ya uchaguzi marekebisho kutoa nafasi ya uchaguzi wa mapema.

Kiongozi wa upinzani Jeremy Corbyn ameunga mkono uchaguzi wa mapema huku akimlaumu Waziri Mkuu kwa kutotekeleza ahadi zake kwa raia.

Ad