Home » Washirika » Mamlaka Ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA)

Mamlaka Ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA)

16 February 2016 | Washirika

UMUHIMU WA KITAMBULISHO

Vitambulisho vya Taifa ni chachu ya maendeleo ya Kiuchumi, kijamii na  kiusalama

1. Vitasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali

2. Vitasaidia kumtambua mhusika kirahisi anapohitaji kupatiwa huduma katika taasisi mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya.

3. Vitarahisisha kuwatambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka kwenye benki na asasi mbalimbali za fedha nchini.

4. Vitasaidia kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari la kumbukumbu la kielektroniki.

5. Vitawezesha kumtambua mtu anapofanya biashara au shughuli nyengine kwa kutumia majina tofauti.

6. Vitafanikisha kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii. Kwa mfano, kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo raia wa Tanzania anastahili kupata kirahisi kwani kupitia kitambulisho mtu atatambulika kirahisi(nani ni nani?, yuko wapi?, na anafanya nini? katika taifa hili.

7. Vitasaidia kuondoa watumishi hewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ‘payroll’ ya Serikali.

8. Vitaimarisha utendaji kazi Serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za watumishi na malipo ya stahili zao, hasa pale wanapostahafu.

9. Vitarahisisha zoezi la kuhesabu watu (sensa).

10. Vitarahisisha zoezi la kuhuisha daftari la wapiga kura, ambapo kwa sasa hufanyika mara mbili kabla ya uchaguzi mkuu.

Ad