Home » Nje Ya Afrika » Vongozi mbalimbali duniani wanaedelea kutuma risala za rambirambi baada ya kuuawa kwa Mbunge wa chama cha Leba Jo Cox

Vongozi mbalimbali duniani wanaedelea kutuma risala za rambirambi baada ya kuuawa kwa Mbunge wa chama cha Leba Jo Cox

17 June 2016 | Nje ya Afrika

Vongozi mbalimbali duniani wanaedelea kutuma risala za rambirambi baada ya kuuawa kwa Mbunge wa chama cha Leba Jo Cox hapo jana aliyepigwa risasi na kudungwa kisu.

Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 41, alishambuliwa wakati alipokuwa katika eneo bunge lake na mwanamume ambaye tayari ameshakamatwa na inadaiwa kuwa alimtamka neno Uingereza kwanza kabla ya kutekeleza shambulizi hiyo.

Bi Hillary Clinton anayewania tiketi ya chama cha Democratic nchini Marekani kuwania urais mwezi Novemba mwaka huu, ni miongoni mwa wale waliotoa risala za rambirambi.

Kuawa kwa mbunge huyu wa upinzani kumesababisha kusitishwa kwa muda kampeni ya kura ya maoni inayitaajiwa kufanyika wiki ijayo kuamua ikiwa nchi hiyo ijiondoekwenye umoja wa ulaya au la

Ad