Home » Tanzania » Amiri Jeshi Mkuu aagiza kikosi cha Nyumbu kuimarishwa

Amiri Jeshi Mkuu aagiza kikosi cha Nyumbu kuimarishwa

25 January 2016 | Tanzania

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais JOHN MAGUFULI ameiagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuimarisha kikosi cha NYUMBU ili kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kutengeneza silaha mbali mbali za kijeshi.

Amiri Jeshi Mkuu ametoa kauli hiyo jijini ARUSHA wakati wa kuhitimisha mafunzo ya zoezi la kuonesha uwezo wa medani katika komandi ya 303 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambapo amesema  ana imani kuwa Jeshi litajipanga vizuri ili kikosi hicho kitekeleze malengo yaliyokusudiwa.

Amesema hivi sasa ipo haja ya kutumia wanajeshi katika kujenga uchumi wa nchi kutokana na uaminifu wao pamoja na nidhamu iliyotukuka.

Kufuatia kazi nzuri waliofanya wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT pamoja na Mgambo katika zoezi hilo la kuonyesha uwezo wa medani, ameagiza wale ambao ni JKT na MGAMBO waajiriwe moja kwa moja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TANZANIA.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk HUSSEIN MWINYI amesema serikali imeonyesha juhudi katika kuwekeza na kuimarisha Jeshi la Kujenga Taifa na kulifanya kuwa na vifaa bora na vya kisasa.

Kwa upende wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jeneral DAVIS MWAMUNYANGE amesema lengo la mazoezi hayo ni kuimarsha uwezo na viwango katika kupanga na kutekeleza ulinzi wa nchi na pia yatakuwa endelevu.

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Januari 23 anatarajia kutoa kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa kijeshi katika chuo cha mafunzo ya kjeshi MONDULI.

Ad