Home » Tanzania » SERIKALI yaombwa kuchangia chakula cha watoto wakiwa shule

SERIKALI yaombwa kuchangia chakula cha watoto wakiwa shule

21 January 2016 | Tanzania
SERIKALI yaombwa kuchangia chakula cha watoto wakiwa shule ili kuwasaidia kusoma wakiwa wameshiba kwani watoto hawawezi kusoma wakiwa na matumbo hayana chakula.
 
Hayo yamesemwa na Shule kuu ya Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Joviter Katabaro wakati akichangia maada katika mkutano wa kujadili masuala ya elimu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyrere jijini Dar es Salaam leo.
 
Nae Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Haki Elimu, John Kalage kuwa wamependekeza Lugha ya Kiswahili na Kiingereza iwe lugha ya kufundishia na kujifunzia kwa ngazi zote ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
 
Pia ametoa wito kwa serikali kuwa kutoa elimumsingi bure sabamba na kupunguza michango ya wazazi mashuleni.
 
Aidha Karage  amesema kuwa ili kuhakikisha ubora mashuleni, shule, taasisi na vyuo vinapaswa kufanyiwa ukaguzi kuhusu ufundishaji na ujifunzania pamoja na mazingira kuwa mazuri.
Ad