Home » Afrika » Baraza la Usalama La Umoja Wa Mataifa kukutana na Rais Nkurunziza

Baraza la Usalama La Umoja Wa Mataifa kukutana na Rais Nkurunziza

26 January 2016 | Afrika

Wajumbe 15 wa Baraza la Usalama La Umoja Wa Mataifa wapo mjini BUJUMBURA nchini BURUNDI ambapo wanatarajia kukutana na Rais PIERRE NKURUNZIZA wa BURUNDI na kufanya mazungumzo nae kuhusu amani ya nchi hiyo.

Mamia ya waandamanaji wanaounga mkono utawala wa Rais NKURUNZIZA walijitokeza nje ya uwanja wa ndege kupinga ujio wa wajumbe wa baraza hilo.

Nchi ya BURUNDI imejikuta katika ghasia baada ya Rais NKURUNZIZA kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa muhula wa tatu na hatimaye kutekeleza azma yake.

Hatua ya Rais huyo ilishutumiwa na upinzani na kutajwa kama ukiukaji wa katiba ya nchi hiyo na hivyo kusababisha maandamano nchini humo kwa miezi kadhaa kupinga jambo hilo.

Hii ni mara ya pili kwa wajumbe wa Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzuru nchi hiyo katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Ad