Home » Tanzania » WAZIRI JAFO AELEKEZA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UPANDAJI MITI TANZANIA

WAZIRI JAFO AELEKEZA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UPANDAJI MITI TANZANIA

13 August 2022 | Tanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhusisha masharti ya upandaji miti kwa vibali vya ujenzi.

Ametoa maelekezo hayo  Agosti 11, 2022 wakati akishiriki uzinduzi wa kampeni ya ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyokwenda sambamba na zoezi la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika eneo hilo mara baada ya matembezi ya hisani, Dkt. Jafo alipongeza Wizara ya Madini na shirika hilo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira.

Alisema ili kuwa na dhamira ya dhati katika utunzaji wa mazingira na kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika zinazoyakabili maeneo mbalimbali nchini wakurugenzi wanapogawa viwanja wahakikishe vinakuwa na eneo la kupanda miti.

Ad