Home » Tanzania » Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kusudio la kuunda kamati ya wataalamu watakaoshauri juu ya mustakabali wa kukabiliana na corona.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kusudio la kuunda kamati ya wataalamu watakaoshauri juu ya mustakabali wa kukabiliana na corona.

06 April 2021 | Tanzania

Rais wa Tanzania kuunda kamati ya wataalamu kumshauri

Rais Samia amesema Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa katika janga hilo la corona ambalo linaitikisa dunia kwa mwaka mmoja uliopita.

 

"Suala la Covid 19 nakusudia kuunda kamati ya kitaalamu. Halifai kulinyamazia bila kufanya tafiti ya kitaalamu. Watuambie upeo wa suala hili... Sio ikitajwa Tanzania basi inakuwa deshi, deshi...Hatuwezi kujitenga kama kisiwa," ameeleza rais Samia.

 

Rais Samia ameyasema hayo hii leo katika Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam baada ya kuwaapisha Makatibu Wakuu wa Wizara na wakuu wa mashirika

 

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kusudio la kuunda kamati ya wataalamu watakaoshauri juu ya mustakabali wa kukabiliana na corona

 

/BBC

Ad