Home » Afrika » Tume ya uchaguzi Kenya imejipanga upya kuharakisha ujumlishaji wa matokeo ya kura za urais

Tume ya uchaguzi Kenya imejipanga upya kuharakisha ujumlishaji wa matokeo ya kura za urais

14 August 2022 | Afrika

 

Ikiwa ni siku ya Tano sasa wakenya wakisubiri kwa hamu na ghamu kumjua rais wao mpya, Tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC imelazimika kubadili mpango wake wa kazi ilikuharakisha ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi wa urais mbali na kuhakiki stakabadhi zinazotoka katika maeneo yote nchini.

Mwenyekiti wa IEBC bwana Wafula Chebukati amekiri mwendo wa kupokea na kuhakiki matokeo hayo ya urais umekuwa wa kasi ya chini mno huku afisa mmoja akihitaji kati ya saa tatu na nne kuhudumiwa katika kituo cha kitaifa cha uchaguzi cha ukumbi wa Bomas Nairobi.

"Tume ya IEBC imegundua kuwa tunachukua kati ya saa 3 - 4 kukamilisha mchakato wa kupokea matokeo kutoka kwa afisa aliyesimamia uchaguzi katika eneo bunge moja. Tuna baadhi ya maofisa ambao wamekaa kwenye viti hivi kwa siku tatu. Maafisa 265 wameripoti. Tumefaulu kuwashughulikia 141 na kusalia na 124 ambao bado wako kwenye foleni'' Alisema Chebukati.

" Tunataka kufanya marekebisho yafuatayo: Wasimamizi wa uchaguzi watakabidhi fomu zao asili 34A kwa afisa wa kitaifa wa kujumlisha mara tu baada ya tangazo hili.Watatoa ripoti kwa dawati la TEHAMA, kwa uthibitisho wa matokeo yaliyotumwa dhidi ya Fomu 34A

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea nchini Kenya baada ya raia wake kushiriki katika uchaguzi mkuu siku ya Jumanne.

Ad