Home » Video » VIDEO: Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea Seif Shariff Hamad

VIDEO: Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea Seif Shariff Hamad

News Category: 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad, katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam, ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelzwa kwa matibabu.

Pamoja na kumpa mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif Shariff Hamad kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

"Nilishtushwa sana na taarifa za kuugua kwako, lakini sasa nafurahi kukuona ukiwa mwenye afya nzuri ikilinganishwa na taarifa nilizozipata hapo awali, nakupa pole sana" amesema Rais Magufuli wakati akimjulia hali hotelini hapo.

Kwa upande wake Maalim Seif Shariff Hamad amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu na upendo aliouonesha kwa kumtembelea hotelini hapo, na amewahakikishia watanzania kuwa hali yake sasa inakwenda vizuri na inazidi kuimarika kila kukicha.

"Sasa hivi ninaweza kutembea vizuri, kufanya shughuli zote mwenyewe bila ya msaada wa mtu yeyote yule, na ni matumaini yangu kwamba baada ya muda mfupi, hali yangu itarudi kama kawaida, nije nishirikiane na watanzania wenzangu katika kutekeleza majukumu ya nchi yetu" Maalim Seif alimweleza Rais Magufuli.

 

Ad