Home » Afrika » Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kushirikiana na Chuo Kikuu cha Komoro

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kushirikiana na Chuo Kikuu cha Komoro

21 January 2016 | Afrika

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini mkataba wa makubaliano juu ya mashirikiano na Chuo Kikuu cha Komoro mjini Moroni katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 19 Januari, 2016 na kuhudhuriwa na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Komoro, Balozi wa Komoro nchini Tanzania Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Bw Mudrik Ramadhan Soragha.

Makubaliano kati ya vyuo hivi ni moja ya matokeo ya ziara ya nchini Komoro ya Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoifanya hivi karibuni.

 

CHUO KIKUU CHA TAIFA (SUZA)

Sanduku la Posta 146, Zanzibar - Tanzania

Simu: + 255 24 2230724/2233337/2234063 Nukushi: + 255 24 2233337

Barua pepe: Tovuti:

Ad