Home » Afrika » Kuwekewa vikwazo kwa rais wa Sudani Kusin

Kuwekewa vikwazo kwa rais wa Sudani Kusin

27 January 2016 | Afrika

Jopo la wataalam wa Umoja wa mataifa wamependekeza kuwekewa vikwazo kwa rais wa Sudani Kusin , kiongozi wa waasi na maafisa wengine wawili kwa kuhusika katika vita ya kikatili nchini humo, wanadiplomasia wamesema jana Jumanne.

Orodha ya majina manne imefikiswa kwenye baraza la Usalama la Umoja wa mataifa katika waraka wa siri wa nyongeza kwenye ripoti ya jopo hilo ambayo pia inapendekeza kuwekwa kwa vikwazo vya kuingiza silaha nchini Sudan Kusini.

Rais Slva Kiir , kiomgozi wa waasi Riek Machar mkuu wa majeshi Paul Malong na mkuu wa usalama wa ndani Akol Koor, wameorodheshwa kwa mfululizo wa ukiukaji mkubwa wa haki, kwa mujibu wa wanadiplomasia wanaofahamu kuhusu ripoti hiyo.

Ad