Home » Afrika » Rais wa Kenya, kuwaondoa watumishi wa Mungu waongo

Rais wa Kenya, kuwaondoa watumishi wa Mungu waongo

18 January 2016 | Afrika

Rais wa Kenya Uhuru Mwigai Kenyatta ameendelea kusisitiza azma ya Serikali ya kutaka kuwashughuikia na kuwaondoa watumishi wa Mungu waongo ambao wanatumia udhaifu wa raia kujilimbikizia mali kupitia sadaka.

Rais Kenyatta ameyasema haya akiwa mjini Mombasa, ambapo amewataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali katika kuwabaini wanaojiita watumishi wa Mungu lakini wamekuwa wakitumia mgogngo wa kanisa kujinufaisha.

Licha ya kuunga mkono wazo la viongozi wa dini kutaka wao ndio wajifanyie tathmini, rais Kenyatta anasema lazima kuwe na sheria ambazo zitawabana watumishi feki wanaowahadaa wananchi ambao wengi wanamahitaji ya kiroho.

Ad