Home » Afrika » Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anawataka wakenya kuwafichua Magaidi

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anawataka wakenya kuwafichua Magaidi

07 January 2016 | Afrika

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anawataka wazazi na jamii kwa jumla kushirikiana na serikali na kuwafichua vijana wanaojiunga na makundi ya kijihadi au kwenda kujiunga na kundi la Al Shabab nchini Somalia.

Akizungumza na vijana kutoka majimbo ya Pwani mjini Mombasa, rais Kenyatta amesisitiza kuwa kuwaficha wahalifu kutasaidia kuhatarisha maisha ya wakenya.

Usalama umekuwa ukiimarishwa mjini Mombasa kwa hofu kuwa vijana wengi wamejiunga na kundi la Al Shabab ambalo limeendelea kutishia usalama wa Kenya kutokakana na jeshi lake kuwa nchini Somalia

Ad