Home » Afrika » Serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya itapendekezwa ndani ya siku 10

Serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya itapendekezwa ndani ya siku 10

27 January 2016 | Afrika

Serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya itapendekezwa ndani ya siku 10 afisa mmoja amesema jana Jumanne , baada ya bunge la serikali inayotambuliwa kimataifa kupinga ile ya awali, hatua ambayo ni pigo kubwa katika juhudi za amani.

Mataifa yenye nguvu yamezitaka pande hasimu nchini Libya kuunga mkono serikali ya Umoja wa kitaifa iliyoundwa juma lililopita chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa , kwa lengo la kumaliza mkwamo wa kisiasa ambao umechochea kuibuka kwa makundi ya kijihadi.

Siku ya Jumanne Vyanzo vya Ulaya vilisema wajumbe 28 wa Umoja wa Ulaya wanafikiria kuchukua hatua ya kuweka vikwazo dhidi ya wale wanao onekana kuvuruga juhudi za kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Ad