Home » Afrika » Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni inaendelea nchini Somalia

Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni inaendelea nchini Somalia

18 January 2016 | Afrika

Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni maalumu ya utafutaji na uokoaji inaendelea nchini Somalia siku chache tu baada wanamgambo wa Al-Shabab kutekeleza shambulizi la kushtukiza kwenye kambi moja ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika na kudai kuwaua zaidi ya wanajeshi 100.

 

Kambi hiyo iliyoko kusino magharibi mwa nchi ya Somalia ilivamiwa na wanamgambo hao alfajiri ya siku ya Ijumaa, ikiwa ni shambulio jingine baya zaidi kutekelezwa na wanamgambo hao wakilenga kambi ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

Ad