Home » Afrika » Umoja wa Mataifa umetuma mialiko kwa ajili ya mazungumzo mapya ya amani nchini Syria

Umoja wa Mataifa umetuma mialiko kwa ajili ya mazungumzo mapya ya amani nchini Syria

27 January 2016 | Afrika

Umoja wa Mataifa umetuma mialiko kwa ajili ya mazungumzo mapya ya amani nchini Syria yatakayofanyika mjini Geneva Uswisi juma hili, huku wawakilishi wa upinzani wakijadili kuhusu kuhudhuria au la.

Mialiko imetolewa huku vikosi vya serikali kwa kusaidiwa na ndege za kivita za Urusi vikifanikiwa kuuteka mji wa waasi kusini mwa Syria , katika ushindi wao wa karibuni tangu Moscow ilipoanza kampeni ya mashambulizi ya anga mwezi Septemba mwaka jana.

Ofisi ya Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura imesema kuwa imetoa mialiko kwa ajili ya mazungumzo hayo ambayo yamepangwa kuanza siku ya Ijumaa, bila kusema nani wamealikwa.

Ad