Home » Katiba » KATIBA INAYOPENDEKEZWA - UTANGULIZI

KATIBA INAYOPENDEKEZWA - UTANGULIZI

06 January 2016 | Katiba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alianzisha mchakato wa uandikaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2011 kutokana na maombi ya wananchi wakiwemo viongozi wa vyama vya Siasa walioonyesha uhitaji wa Katiba mpya inayoendana na mazingira ya sasa ya nchi yetu.

Mchakato huu umekamilika na kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni ya mwaka 2013, taifa linasubiri kupiga kura ya maoni hapo Aprili 30, 2015 ya kufanya uamuzi wa kuikubali au kuikataa Katiba Inayopendekezwa.

Lengo la kutumia njia hii ya Mawasiliano ni kuwapa nafasi wananchi ya kupata eimu kwa umma juu ya maudhui ya Katiba Inayopendekezwa kwa lugha nyepesi kupitia makala, habari katika picha, vipindi vya Radio na Teevisheni, michezo ya kuigiza katuni pamoja na kupokea maswali na maoni ambayo yatajibiwa na wataalam wenye uelewa juu ya Sheria na masuala ya Katiba.

Chombo hiki kimeandaliwa na kuratibiwa na watanzania wenye ujuzi wa masuala ya Habari na Mawasiliano kwa kushirikiana na wanaharakati wa masuala ya Katiba kwa lengo kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilichomo kwenye Katiba Inayopendekezwa kwa faida ya watanzania wote kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi wakati wa upigaji wa kura ya maoni.

Ad