Home » Makala » Kituo cha afya cha Luchelengwa kupewa gari la kubebea wagonnjwa pamoja na mashine ya kisasa ya Xray

Kituo cha afya cha Luchelengwa kupewa gari la kubebea wagonnjwa pamoja na mashine ya kisasa ya Xray

21 December 2018 | Makala

SERIKALI-YAAHIDI-NEEMA-SEKTA-YA-AFYA-RUANGWA

Katika kuhakikisha inawajali wananchi wake na kuboresha huduma za afya nchini, Serikali ya awamu ya Tano imeahidi kukipatia kituo cha afya cha Luchelengwa gari la kubebea wagonnjwa pamoja na mashine ya kisasa ya Xray kabla ya Aprili 2019.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema hayo alipokuwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa alipokuwa anapokea taarifa ya Afya ya Wilaya Desemba 20.

Mheshimiwa Ummy alitoa ahadi hizo baada ya Mkuu wa Wilaya kutaja changamoto hizo zinazosabababisha kusuasua kwa upatikanaji wa huduma ya afya ya uhakika.

" mwezi wa 3 mwakani nitakabidhi gari la kubebea wagonjwa kituo cha Afya luchelengwa na nitakabidhi mwezi wa 2 machine ya mionzi ya kisasa mwezi wa 2" amesema Waziri wa Afya

Hivyo Waziri alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuanza ujenzi mara moja wa chumba cha kisasa cha kuhifadhia machine ya mionzi katika hospital ya Wilaya ili iwe rahisi kukabidhi mashine hizo kwa wakati.

Pia aliupongeza uongozi wa Hospital ya Wilaya kwa kujitahidi kuwa na dawa zote za muhimu zinazotakiwa kupatikana hospital baada ya kukagua na kuona stoo ya dawa zilizopo hospitalini hapo.

"Nimefurahishwa na uwingi wa dawa uliopo hospitalini niwatake muendele hivi hivi kuwa na dawa za muhimu za kutosha ili tupunguze suala la wananchi wetu kununua dawa kwenye maduka ya nje ya watu binafsi" amesema Mheshimiwa Ummy.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa  alitoa shukurani kwa serikali  kwa kuahidiwa kupatiwa Gari la wagonjwa na mashine ya mionzi (XRAY).

Pia aliwataka madaktari kuhakikisha kila siku asubuhi wanabadili chati ya dawa ili iwe rahisi katika utendaji wao na kujua dawa ipi ipo kwa siku hiyo na ipi haipo.

" Mara nyingi nimekuwa nikipita naona hamfanyi mabadiliko ya chati ya dawa hii inasababisha wagonjwa kuandikiwa dawa zisizokuwepo kuweni na taratibu kila siku asubuhi kubadilisha itawasaidia sana katika utendaji wenu" amesema Mgandilwa

Ad