Home » Makala » Ukweli kuhusu hali ya mtu baada ya kupata chanjo ya Covid-19 unaweza kuambukizwa tena

Ukweli kuhusu hali ya mtu baada ya kupata chanjo ya Covid-19 unaweza kuambukizwa tena

02 April 2021 | Makala
 • Athari ambazo zinaweza kuwaathiri zaidi ya watu watano kati ya watu 10 baada ya kupokea dozi za Oxford-AstraZeneca vaccine au Pfizer-BioNTech

Baadhi ya watu hujihisi kuumwa baada ya kuchanjwa chanjo ya virusi vya corona - lakini hilo ni jambo la kawaida na ambalo linatarajiwa, wanasema madaktari.

Zaidi ya mtu mmoja kati ya watu 10 anaweza kuhisi adhari baada ya kuchanjwa, ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa, uchovu na kuvimba sehemu ulipochomwa sindano ya chanjo. Lakini watu hawapaswi kuzuiwa kupata chanjo, ambayo inayanusuru maisha yao, wanasema madaktari wa Uingereza. Athari za baada ya chanjo anazozipata mtu huwa ni maumivu kidogo na huwa zinapotea katika kipindi cha siku chache tu, wataalamu wanasema.Lakini athari hizi wakati mwingine zinaweza kumfanya mtu ahisikuumwa sana.
David Kidd, mwenye umri wa miaka 49, kutoka Yorkshire nchini Uingereza ambako watu walianza kupewa chanjo mapema, anasema hakuwa amejiandaa kabisa kuathirika na dalili muda mfupi baada ya kupata dozi yake ya kanza ya Covid. Anasema: "Nilisikia kwamba kulikuwa na uwezekano wa kupata baadhi ya dalili za kuugua ," anasema.

"Wanasema unaweza kupata dalili fulani kama mafua lakini sikutegemea kupata dalili za magonjwa tofauti kwa pamoja.

"Nilichomwa sindano ya chanjo saa sita mchana Jumamosi na hadi saa kumi na mbili jioni." Bwana Kidd alikuwa na :

 • Maumivu ya mwili
 • Mafua
 • Maumivu ya kichwa
 • Macho yalivimba
 • kichefuchefu
 • kupanda kwa joto la mwili
 • Alihisi baridi kali mwilini

"Nilihisi kana kwamba nilikuwa nimetumbukiza mikono yangu kwenye barafu iliyoganda au friji ," anasema

"Yalikuwa maumivu makali kusema kweli na kichwa change kilikuwa kinagonga . Yalikuwa ni maumivu mabaya ya kichwa niliyowahi kuyapata katika maisha yangu yote.

"Na macho yangu yalikuwa kama yanaungua, na kichefuchefu.

Sikujihisi vyema usiku mzima ."

'Kujiandaa vyema'

Bw Kidd alimeza tembe ya paracetamol na ibuprofen na, kufikia Jumapili jioni, alianza kujihisi vyema.

Na haijamzuia kwenda kupata dozi ya pili.

"Bahati nzuri, nilikuwa ninaumwa katika kipindi cha wikendi Luckily ," anasema . "Kwahiyo haikunitia wasi wasi sana.

"Lakini nitakuwa nimejiandaa vyema wakati ujao, kwa ajili ya kazi yangu kama itatokea.

"Na nitakuwa nimehakikisha nimenunua mahitaji yangu yote ya nyumbani ."

Kuhisi kuumwa

Athari ambazo zinaweza kuwaathiri zaidi ya watu watano kati ya watu 10 baada ya kupokea dozi za Oxford-AstraZeneca vaccine au Pfizer-BioNTech ni pamoja na:

• Kuvimba, maumivu, joto, na kujikuna katika eneo ulipochanjwa

• Kuhisi kuumwa kwa ujumla

• Kuhisi uchovu

• Kuhisi baridi mwilini au kupanda lwa joto la mwili

• Maumivu ya kichwa

• Kuhisi kichefuchefu

• Maumivu ya viungo au misuli

Athari zinazoathiri mtu hadi mmoja tai ya watu 10 ni pamoja na:

• Kuvimba sehemu uliyochomwa sindano

• Joto la mwili kupanda

• Kuhisi kuumwa kutokana na (kutapika) au kuharisha

• Kupata dalili kama za mafua, kama vile kupanda kwa joto la mwili, kuvimba kooni, kutiririka kwa makamasi, kikohozi na kuhisi baridi mwilini

 

Usaidizi wa kimatibabu

Profesa Martin Marshall, kutoka taasisi ya College of GPs, anasema "Wagonjwa wanapaswa kuelewa kuwa chanjo zote za Covid-19 zimepitia mchakato wa kuhakikisha zote ziko salama na zina ufanisi.

"Ni kawaida, kama ilivyo kwa chanjo nyingine, kwa baadhi ya wagonjwa kupata dalili za athari kwa kiwango kidogo.

"Kama itahitajika, tunashauri kwamba wagonjwa watibu athari hizi kwa dawa za kuzuia maumivu, kama vile paracetamol."

'Ulinzi wa juu zaidi'

Kwa sasa , takwimu kutoka utafiti wa  - ambayo ilipokea maoni ambayo yalitumwa kwa njia ya programu ,kutoka kwa watu zaidi ya 280,000 - walikuwa wanaonekana kuwa na uchovu, maumivu ya kichwa na kuhisi baridi :

 • wanawake
 • vijana
 • wale walikuwa na Covid

Vijana na wanawake zaidi ya wanaume ndio wanapata madhara kutokana na chanjo hiyo kwasababu wana mfumo mzuri wa kinga, alisema mwanasayansi Prof Tim Spector, wa chuo cha King's College London.

Na wale ambao wanapata madhara wanaweza kupata ulinzi wa juu zaidi hata kwa dozi moja tu ya chanjo - ingawa watu wanashauriwa kupata dozi mbili za chanjo.

"Kama mtu alipata corona kabla , wanakuwa tayari kutumia," alisema.

"Na miili yao iko tayari kupambana nayo tena."

Kadi ya njano ya data, ingawa inaonesha uhusiano kati ya madhara ya maambukizi ya Corona na athari zinazoweza kujitokeza baada ya kutumia chanjo.

Lakini inalenga kurekodi athari yoyote kali kuliko zile ndogondogo.

Na wizara ya afya Uingereza inawataka watu waliopata Corona kupata chanjo bado ili kujilinda wenyewe na kuwalinda wengine.

Prof Spector alisema: "Unaweza ukaumwa kidogo tofauti na ukipata Covid.

"Usichelewe kupata chanjo au kuacha kupata dozi hiyo ya chanjo.

 

/BBC