Home » Nje Ya Afrika » Donald Trump apata ushindi katika majimbo mawili nchini Marekan

Donald Trump apata ushindi katika majimbo mawili nchini Marekan

09 March 2016 | Nje ya Afrika

Donald Trump amewaacha vinywa wazi wale wanaompinga Jumanne hii kwa ushindi alioupata katika majimbo mawili nchini Marekani katika kura za mchujo kwa kuwania urais kupitia bendera ya chama cha Republican.

 

Wakati huo huo Hillary Clinton anayewania urais kwa tiketi ya chama cha Democratic ameangushwa na mshandani wake Bernie Sanders dhidi ya matokeo katika jimbo la Michigan, huku Hillary Clinton akiibuka mshindi katika jimbo la Mississipi.

Mgombea anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amejiongezea ushawishi kama mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na Mississippi.

Katika jimbo la Mississippi, Donald Trump amepata kura 47% dhidi ya mshindani wake Ted Cruz, ambaye amepata 36%.

Baada ya kupata ushindi huo, Trump amesema kuwa anakiongezea umaarufu chama cha Republican.

Ted Cruz ameimarisha nguvu zake za kushikilia nafasi ya pili katika chama cha Republican kwa kushinda kura za mchujo katika katika jimbo la Idaho, kaskazini magharibi mwa Marekani. Matokeo ya kura za mchujo wa nne yamekua yaksubiriwa katika jimbo la Hawai. Seneta Florida Marco Rubio amepata matokeo mabaya, na hivyo kumaliza wa mwisho katika majimbo ya Michigan na Mississippi.

Ushindi huu mara mbili wa Donald Trump umezima uvumi wa mwishoni mwa juma lililopita kuwa kampeni yake ilikuwa imepoteza kasi.

Ad