Home » Nje Ya Afrika » Fahamu familia isiyokuwa na alama za vidole

Fahamu familia isiyokuwa na alama za vidole

29 December 2020 | Nje ya Afrika

Apu Sarker alionesha viganja vya mikono kwa njia ya video akiwa nyumbani Bangladesh. Mara ya kwanza hakuna kilichoonekana tofauti lakini baada ya kutazamwa kwa karibu, ikaonekana mkono wake hauna ala zozote vidoleni.

Apo, 22, anaishi na familia yake katika kijiji cha kaskazini mwa mji wa Rajshahi. Alikuwa akifanyakazi kama muuguzi msaidizi hadi hivi karibuni. Walirithi tatizo hilo kutoka kwa baba yake na babu yake.

Wanaume wa familia ya Apu walionekana kuwa na tatizo sawa la mabadiliko ya chembe za urithi ambao unasemekama ni nadra sana kote ulimwenguni: hawana alama za vidole.

Wakati huo, babu yake Apu hakuwa na alama za vidole lakini wakati wake haikuonekana kuwa shida. "Sidhani kama kuna wakati alianza kuichukulia hali hiyo kama tatizo," Apu amesema.

 

Lakini miongo kadhaa baadaye, alama za vidole zimekuwa zikitumika katika upigaji wa kura, ni lazima kuchukuliwa alama hizo unapotaka kupita katika uwanja wa ndege na hata katika utumiaji wa simu za kisasa za mkononi.

Mwaka 2008, Apu alikuwa bado kijana mdogo wakati Bangladesh ilipoanzisha mfumo wa kupata kitambulisho cha taifa kwa watu wazima ambako kulihitaji alama za kidole gumba.

Maafisa wahusika walishikwa na butwaa wasijue watampa vipi kitambulisho baba yake Apu, Amal Sarker ambaye hana alama za vidole.

Mwaka 2010, ilikuwa lazima kuwa na alama za vidole ili uweze kupata pasipoti na leseni za udereva. Baada ya kuhangaika huku na kule, Amal alifanikiwa kupata pasipoti alipoonesha cheti kutoka kwa bodi ya madaktari kuthibitisha kuwa hana alama za vidole.

Ingawa hakuwahi kutumia pasipoti hiyo kwasababu alihofia kungetokea tena matatizo akiwa uwanja wa ndege.

Na pia ingawa kuendesha pikipiki kwake ni jambo la msingi sana kwa kazi yake ya ukulima, hajawahi kupata leseni ya udereva.

"Nililipa ada, nikapita mtihani lakini hawakunipa leseni kwasababu sikuweza kuthibitisha kuwa nina alama za vidole," alisema.

Mwaka 2016, serikali ilifanya iwe lazima kulinganisha alama za vidole na data ya taifa ili mtu aweze kupata kadi ya simu ya mkononi.

"Wakati ninanunua kadi yangu, wahudumu walionekana kuchanganyikiwa, programu yao ilisita kufanyakazi kila nilipojaribu kuweka vidole vyangu ili vioneshe alama za vidole kwenye king'amuzi," Apu alisema.

Apu hakuweza kupata kadi ya simu, na wanaume wote wa familia hiyo sasa hivi wanatumia kadi ya simu ya mama yake.

Hali hii kwa kiingereza inafahamika kama Adermatoglyphia.

Mara ya kwanza kujulikana ilikuwa mwaka 2007 pale Peter Itin, daktari wa ngozi wa Uswizi alipowasiliana na mwanamke mmoja nchini humo aliyekuwa akijaribu kuingia Marekani bila mafanikio yoyote.

Uso wake ulifanana na picha ya kwenye pasipoti lakini maafisa wa forodhani, hawakuweza kupata alama zake za vidole kwasababu hakuwa nazo.

Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, Profesa Itin alibaini kuwa mwanamke huyo na watu wengine nane wa familia yake walikuwa na vinasaba zisizo za kawaida - vidole vyake havikuwa na alama na pia tezi za jasho mkononi mwake zilikuwa chache mno.

Amal and Apu
 

Maelezo ya picha,

Amal na Apu Sarker. "Sio kwamba sina alama kwenye vidole vyangu, ni kitu nilichorithi," Amal amesema.

Inasemekana kuwa mjomba wake, Apu Sarker kwa jina Gopesh, ambaye anaiishi Dhaka, alilazimika kusubiri kwa miaka miwili kupata pasipoti, anasema.

"Nililazimika kusafiri hadi Dhaka mara nne, tano hivi katika kipindi cha miaka miwili kuwashawishi maafisa kuwa sina alama za vidole," Gopesh amesema.

Tatizo la familia hiyo pia linaweza kusababisha ngozi kuwa kavu sana na kupunguza joto kwenye viganja vya mkononi na miguuni.

Apu Sarker's younger brother Anu also inherited the rare gene mutation
 

Maelezo ya picha,

Kijana mdogo wa Apu Sarker Anu pia naye amerithi tatizo hilo

Amal Sarker anasema ingawa hakusumbuliwa sana maishani mwake kwasababu hiyo, mambo yamekuwa magumu kwa watoto wake.

"Hilo sio tatizo langu, ni kitu nilichorithi," amesema. "Lakini mimi pamoja na vijana wangu tunapojipata kwenye matatizo, huwa nahuzunika sana."

Amal na Apu alipata aina fulani ya kadi inayotolewa na serikali ya Bangladeshi baada ya kuwasilisha cheti cha matibabu. Cheti hicho kinatambua data ya retina na utambuzi wa uso.

"Nimechoka kuelezea hali yangu kila wakati. Nimeuliza ushauri kwa wengi lakini hakuna aliyenipa jibu muafaka," amesema Apu. "Yupo mmoja aliyenishauri kwenda mahakamani ikiwa njia zote zitashindikana."

Apu ana imani ipo siku atafanikiwa kupata pasipoti na kusafiri nje ya Bangladesh.

Picha ni kwa hisani ya familia ya Sarker.

/BBC

Ad