WAANDISHI WA AFRIKA JIFUNZENI KUFICHA MABAYA YENU, TANGAZENI MAZURI KWANI YANAYOENDELEA ULAYA NI HATARI MNO

Usiyoyajua kuhusu maandamano ya Ufaransa
Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL
Nchini Ufaransa na katika baadhi ya mataifa ya ulaya kwa mawiki kadhaa sasa tumeshuhudia maandamano makubwa ambayo waliyaita “vizibao vya njano”, tumeshuhudia moto ukiwaka. Vifo pia vilikuwako katika matukio hayo, Nchini Ufaransa mwishoni mwa wiki iliyopita peke yake kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka serikalini mamia ya waandamanaji walijeruhiwa huku maelfu ya waandamanaji wakitiwa nguvuni.
Je nini kimeisibu Ulaya?
Wananchi wa Ulaya wamejifungia na wanaishi kama vile ilivyokuwa kabla ya vita kuu ya 2 ya dunia.
Sababu zinazopelekea upinzani unaoonyeshwa na jamii za ulaya dhidi ya wahamiaji, waislamu, wayahudi na wageni kutoka nchi nyingine. Chanzo cha matatizo sio wahamiaji bali ni jamii zenyewe za Ulaya. Tatizo ni kuhusu mustakabali wa Ulaya, kama tunavyoona kinachojiri hivi sasa. “
Je Ulaya itajenga maadili kupitia Umoja wa Ulaya? Au wataandelea kutumia unazi na ubeberu waliorithi kutoka zama za kale? ”
Kuhusiana na hili tulisisitiza kwamba kama makundi ya watetezi wa uhuru katika jamii za Ulaya yasipopaza sauti zao kulisema hili , itafikia muda watakuwa wamechelewa na wasiweze kufanya chochote.
Matukio ya nchini Ufaransa
Maandamano ya nchini ufaransa ya hivi karibuni unaweza kusema yanatokana na jamii hiyo kujifungia, chuki na ubaguzi kuonekana kitu cha kawaida, na jamii hizo kujali maslahi yao zaidi kuliko kitu chochote.
Matukio ya vizibao vya njano hayakusababishwa na wahamiaji, bali yanatokana na jamii hizo kushindwa kuendana na kasi ya utandawazi, yalitokana na mkwamo wa uchumi, yalitokana na Ufaransa kushindwa kudumisha ustawi wa jamii uliokuwako zamani.
Matukio yanayoendelea duniani hivi sasa pamoja na nguvu nyingine za kiuchumi zinazoibuka, vinaifanya Ufaransa na mataifa mengine ya Ulaya kushindwa kudumisha ustawi wa jamii na kuleta maendeleo.
Matukio na vyombo vya habari
Katika matukio yaliyotokea İstanbul kwenye eneo la Gezi, karibu vyombo vya habari vya dunia nzima viliweka kambi pale walirusha matangazo ya moja kwa moja kwa masaa bila kukoma. Hatuwezi kusahau jinsi vilivyowafanya waandamanaji kuwa mashujaa
Bado yule binti aliyekuwa na kilemba chekundu na alama ya mwanaume aliyesimama vipo kwenye akili zetu. Vyombo vya habari vililikuza tukio vilionyesha kwamba Uturuki na hasa polisi ni wavunjifu wakubwa wa haki za binadamu
Tukirudi katika matukio ya Paris, vyombo vya habari vya Ulimwengu vimeyapa nafasi ndogo sana. Vyombo hivyo havikuripoti vya kutosha nguvu kubwa iliyotumiwa na polisi dhidi wanafunzi wa sekondari walioshiriki maandamano hayo. Havikuonyesha uvunjifu huu wa haki za binadamu.