Home » Tanzania » Gereza la kwitanga na kambi ya JKT Bulombora kuwa vituo vikubwa vya uzalishaji wa miche ya zao la chikichi.

Gereza la kwitanga na kambi ya JKT Bulombora kuwa vituo vikubwa vya uzalishaji wa miche ya zao la chikichi.

17 February 2019 | Tanzania
 
 
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

WAZIRI mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali imechagua gereza la kwitanga na kambi ya JKT Bulombora kuwa vituo vikubwa vya uzalishaji wa miche ya zao la chikichi.

Hayo ameyasema leo kwenye kambi ya bulombora wakati akiongea na wananchi pamoja na vijana wa JKT Bulombora wakati akiwa kwenye siku ya pili ya ziara yake kikazi.

Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa gereza la kwitanga kuongeza nguvu katika uzalishaji wa zao hilo ikiwa ni sambamba na kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha zao la mchikichi.

"Wataalamu wowote kutoka duniani kote watakaotaka kujifunza kilimo cha zao la chikichi tutawaleta hapa Bulombora JKT na gereza la kwitanga pamoja na Ilagala haya maeneo yatatumika kama shamba darasa la zao hilo"alisema Majaliwa

Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Kigoma pamoja na Wilaya zote na halmashauri ambazo zao la chikichi linastawi vizuri kutoa elimu na kuhamasisha wananchi jinsi ya kulima zao hilo kisasa ambapo mbegu(miche)ambapo wananchi watakuwa wanapewa bure kwenye halmashauri husika.

Alisema Wizara ya kilimo wanatakiwa kusimamia maeneo yote ambayo zao la chikichi linalimwa kisasa na wananchi.

"Nimefurahishwa na jitihada zinazofanywa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT)kambi ya hapa Bulombora kwa kuandaa eneo lenye hekta zaidi ya 480 kwaajili ya kilimo cha zao la chikichi lakini hapa malengo yetu ni kulima hekta 2000,Gereza la kwitanga napo nimekuta wanasafisha shamba la hekta 450 na wao wanatakiwa kulima hekta zaidi ya 2000,tulime maeneo tunayo yakutosha"Alisema Waziri Mkuu.

Waziri mkuu amewataka wakulima wakubwa makampuni na taasisi binafsi kuja kuwekeza kigoma kwenye zao la chikichi kwenye vitalu vya mbegu bora,pia watapata maeneo ya kulima ili wawekeze kwenye kilimo chenyewe.

"Kwakweli tukifikia hatua hiyo nchi yetu ya Tanzania hatutakuwa na shida ya kuagiza mafuta ghafi toka nje ya nchi na dola zitabaki ndani"alisema Majaliwa.

Naibu waziri wa Kilimo Mgumba naye alisema tayari Wizara imeshatenga kwenye bajeti shilingi bilioni 10 kwaajili ya uendelezaji wa zao hilo,ambapo kwenye bunge lijalo.

"Mhe.Waziri Mkuu lakini hatuwezi kusubiria hadi hizo bilioni 10 hadi zipitishwe mwezi wa saba tumeanza kujibana matumizi yetu katika bajeti iliyopita ya mwaka jana,ili tuweze kutekeleza azma ya serekali ya kuendeleza zao la mchikichi nchini na kumaliza tatizo la mafuta"alisema Naibu waziri wa Kilimo

Alisema mpaka sasa wameshapeleka watumishi wawili waliobobea katika utafiti wa zao hilo katika kituo cha utafiti cha Kihinga na ndani ya wiki hii watakuja watafiti wengine 10 kutoka vyuo mbalimbali vya utafiti wa zao mchikichi na kwenda Kihinga.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini Peter Serukamba alimwambia Waziri Mkuu changamoto inayowakabili wakulima wa zao hilo ni upatikanaji wa mbegu bora,hivyo aliiomba serikali wakulima wapate mbegu bora na za kisasa pi matumizi hafifu ya teknolojia ya kilimo hicho.

 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akizindua matreka mawili katika gereza la kwitanga ambayo yatatumika katika  shamba la Kwitanga kuendeleza za la chikichi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama mikungu ya zao la chikichi iliyochavushwa kitaalam ili kupata mbegu bora wakati alipotembelea kituo cha utafiti wa michikicho cha Kihinga Kilichopo Wilayani Kigoma
 

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mche wa zao la chikichi katika shamba la JKT Bulombora ikiwa ni uhamasisha wa kulima zao hilo na kulifanya zao la kimkakati.

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akipanda mche wa zao la chikichi kwenye shamba la JKT Bulombora katika kuhamasisha kulima zao hilo