Rais Magufuli Afungua Rasmi Maktaba Mpya UDSM
01 December 2018 | Tanzania November 27, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha wanaoshuhudia ni Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, leo Novemba 27, 2018, anatarajiwa kuzindua Maktaba ya Kisasa na Kituo cha Kichina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam almaarufu kama UDSM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja huku viongozi wengine wakipiga makofi.
Maktaba hiyo ya kisasa na Kituo cha Kichina vinavyozinduliwa kesho vipo kwenye eneo la mita za mraba 20,000. Katika Maktaba hiyo, pamoja na mambo mengine, kuna sehemu za kujisomea, kuhifadhi vitabu, ofisi za wafanyakazi na ukumbi wa kisasa wa mihadhara na mikutano.
Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli ndiye aliyeweka jiwe la msingi katika ujenzi huo uliofanywa na Kampuni ya Kichina ya Jiangsu Jiangdu. Kupitia ufunguzi huo, Rais Magufuli anataongea na Taifa kutokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
#000000">Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya kitabu kilichomo katika Maktaba hiyo mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla hajaifungua rasmi huku Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akitazama.
#000000">Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akirudisha kitabu hicho kwenye shelfu la vitabu mara baada ya kukisoma huku Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akiangalia. 
#000000">Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya kompyuta zinazohifadhi vitabu (onlinebooks) ambazo wanafunzi watakuwa wakijisomea pamoja na kupata huduma ya mtandao internet.
#000000">Taaswira ya moja ya Mashelfu yenye vitabu katika maktaba hiyo mpya.






