Home » Tanzania » Taarifa ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Makinikia

Taarifa ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Makinikia

12 June 2017 | Tanzania

MUHTASARI WA RIPOTI YA KAMATI MAALUM YA
KUCHUNGUZA MASUALA YA KISHERIA NA KIUCHUMI
KUHUSIANA NA MCHANGA WA MADINI UNAOSAFIRISHWA
NJE YA NCHI

Utangulizi
Mheshimiwa Rais,
Kama ambavyo Watanzania watakumbuka tarehe 10 Aprili
2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt
John Pombe Joseph Magufuli aliteua Kamati Maalum ya
Kuchunguza Masuala ya Kisheria na Kiuchumi Kuhusiana na
Mchanga wenye Madini unaosafirishwa nje ya nchi
yakiwemo makontena 277 yaliyozuiliwa na Serikali katika
Bandari ya Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ni:
1. Prof. Nehemiah Eliakim Osoro (Mwenyekiti)
2. Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara
3. Dr. Oswald Joseph Mashindano
4 Bw. Gabriel Pascal Malata
5. Bw. Casmir Sumba Kyuki
6. Bi. Butamo Kasuka Philip
7. Bw. Usaje Benard Asubisye
8. Bw. Andrew Wilson Massawe

2
Mheshimiwa Rais,
katika kutekeleza uchunguzi huo, Kamati Maalum iliongozwa
na Hadidu za Rejea zifuatazo:
1. Kufanya tathmini ya mchakato mzima wa usafirishaji
wa makinikia na kujiridhisha iwapo utaratibu huo
unafanyika kwa mujibu wa Mikataba iliyoingiwa baina
ya Serikali na Makampuni ya uchimbaji wa madini
“Mining Development Agreements” (MDAs) na
“Special Mining Licence” (SPL) na kwamba taratibu
hizo zinafuatwa kikamilifu. Pamoja na masuala
mengine ambayo Kamati itaona ni muhimu
kuyafuatilia, Kamati ijiridhishe kuhusu mrejesho wa
taarifa za uchenjuaji wa makinikia kutoka nje ya nchi
kwa mamlaka za Serikali.
2. Kupitia Mikataba husika na kushauri endapo
inazingatia kikamilifu maslahi ya nchi ama inahitaji
kuboreshwa. Maeneo yenye mapungufu na
mapendekezo ya maboresho yabainishwe wazi.
3. Kufanya tathmini ya mfumo mzima wa udhibiti kuhusu
biashara ya makinikia kutoka kuchimbwa, kusafirishwa,
kuyeyushwa na kuuzwa kwa madini yanayopatikana
katika makinikia hayo kwa lengo la kubainisha ufanisi
wa mfumo huo katika kuzuia upotevu wa mapato ya
3
Serikali yanayotokana na usafirishaji wa makinikia nje
ya nchi.
4. Kupitia taarifa ya Kamati ya Wataalam ya
kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo
kwenye makontena yenye makinikia ya dhahabu
yaliyokusudiwa kusafirishwa nje ya nchi, iliyoteuliwa
tarehe 29 Machi 2017, hususan, kuhusu aina, kiasi,
viwango vya ubora na thamani za madini yaliyomo
kwenye makinikia hayo na kubainisha kama Serikali
inapata mapato stahiki ya kikodi kutokana na
biashara hiyo kwa mujibu wa mikataba na sheria za
nchi.
5. Kubaini idadi ya makontena yenye makinikia
yaliyosafirishwa kutoka katika migodi ya dhahabu
kuanzia mwaka 1998 hadi sasa; na kwa kuzingatia
taarifa ya Kamati ya Wataalam iliyotajwa katika aya
ya 4, Kamati ifanye makadirio ya kiasi cha mapato
ambacho Serikali ingestahili kupata na kulinganisha na
kiasi halisi cha mapato kilichopatikana katika kipindi
hicho.
6. Kubaini na kujiridhisha kama kuna sababu zozote za
msingi za kiuchumi na kiufundi zinazokwamisha
uanzishwaji wa kiwanda cha kuyeyusha makinikia
4
nchini na kuishauri Serikali ipasavyo. Taarifa hiyo
ibainishe:
i. Nini kinahitajika ili teknolojia ya kuchenjua
mchanga kuwepo hapa nchini;
ii. Ni gharama kiasi gani zinahitajika ili kuanza
uchenjuaji wa makininkia hapa nchini;
iii. Inachukua muda gani kukamilisha ujenzi wa
mtambo husika hadi kuanza kufanya kazi;
iv. Nchi ina uwezo au mapungufu gani katika
kulitekeleza hilo hasa katika upande wa
wataalam na uwekezaji.
(v) Aidha, Kamati ibainishe na kujiridhisha kuhusu
hatua zilizochukuliwa na kampuni za
uchimbaji dhahabu nchini katika kutekeleza
sera na sheria za nchi kuhusu uanzishwaji wa
kiwanda cha kuchenjua makinikia.
7. Kuchunguza na kulinganisha taarifa za uchunguzi wa
kimaabara wa makinikia zinazotolewa na kampuni ya
SGS Tanzania Superintendence Company LTD
(maabara binafsi inayopima sampuli za makinikia ya
kampuni za madini) na Wakala wa Uchungzi wa Madini
Tanzania (Tanzania Mineral Audit Agency –TMAA).
Aidha, Kamati ibainishe ushiriki na majukumu ya
kampuni nyingine ikiwamo SGS kuhusu makinikia.
5
8. Kubainisha uwepo wa mikataba na maudhui yake kati
ya kampuni za uchimbaji madini ya dhahabu Tanzania
na kampuni za uchenjuaji wa makinikia
yanoyosafirishwa ili kijiridhisha kuhusu uhalali wa
biashara hiyo na kama kodi na tozo mbalimbali za
Serikali zililipwa ipasavyo.
9. Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na
mchakato mzima wa usafirishaji wa makinikia, na kutoa
mapendekezo ya kuboresha taratibu husika kwa siku
zijazo kwa maslahi ya nchi.
10. Kufanya kazi kwa karibu na wataalamu katika Sekta ya
Madini waliobobea katika taaluma zao wakiwemo
Wanajiolojia, Wahandisi wa uchenjuaji (Metallurgists),
Wakemia (Chemists), Wataalamu wa masuala ya
Fedha na Wachumi pamoja na wataalam wa masuala
ya sheria na kodi, kadri itakavyoona inahitajika.
11. Endapo itafaa, kuongeza Hadidu za Rejea katika
kuboresha utekelezaji wa majukumu yake. Aidha,
Kamati itakuwa na mamlaka ya kumwita mtu yeyote
au kuwasiliana na ofisi yoyote ya Serikali (kupitia Ofisi ya
Katibu Mkuu Kiongozi) kwa lengo la kupata taarifa
muhimu zinazohitajika.
6
Utekelezaji wa Majukumu
Mheshimiwa Rais,
Katika kutekeleza uchunguzi huo, Kamati ilifanya mambo
yafuatayo:
1. Kuandaa Mpango Kazi, kukusanya na kupitia
mikataba, sheria, sera za madini na kodi, hususan
mikataba ya utafiti, uchimbaji, usafirishaji na uuzaji wa
madini na makinikia, kuchambua na kuhakiki mfumo
mzima wa udhibiti wa biashara ya makinikia, na taarifa
kupokea taarifa kutoka mamlaka za Serikali nchini na
nje ya nchini kuhusiana na uchenjuaji wa makinikia.
2. Kutembelea na kupata taarifa kutoka sehemu na
taasisi zifuatazo:
i. Migodi ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Acacia
Gold Mining Plc), Pangea Gold Mine Ltd (Acacia
Gold Mining Plc), North Mara Gold Mine Ltd
(Acacia Gold Mining Plc), Geita Gold Mine Ltd
(AngloGold Ashanti Ltd);
ii. Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa lengo la kuona
na kupima uzito wa makontena 277 yenye
makinikia yaliyozuiliwa na Serikali; na
iii. Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ofisi Kuu ya
Takwimu, Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa
7
Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA), Shirika la
Madini Tanzania(STAMICO) na Ofisi ya Msajili wa
Makampuni (BRELA), Mamlaka ya Masoko ya Hisa
na Mitaji (CMSA);
3. Kuwaita na kufanya mahojiano na:
i. Watendaji wakuu Serikalini na watumishi wa
taasisi za Serikali na binafsi; na
ii. Watu binafsi wenye ujuzi na uzoefu katika sekta ya
madini, usafirishaji wa mizigo na wakala wa meli.
4. Kupata taarifa na kujifunza kutoka kwenye nchi
nyingine zilizofanikiwa katika biashara ya madini na
uchenjuaji wa makinikia.
5. Kukusanya na kufanya uchambuzi wa takwimu za
makontena ya makinikia yaliyosafirishwa nje ya nchi na
takwimu za kiuchumi na kodi ili kubaini kodi halisi
iliyolipwa na kodi ambayo ilipaswa kukusanywa
kutokana na biashara ya uuzaji wa makininkia nje ya
nchi kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2017.
6. Kufanya uchambuzi kuhusu uwezekano wa ujenzi wa
kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia nchini.
7. Kufanya uchambuzi wa taarifa za kimaabara za
makinikia zilizotolewa na kampuni ya maabara binafsi
inayopima sampuli za makinikia ya madini (SGS),
8
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na
Kamati Maalum Namba 1.
Matokeo ya Uchunguzi
Mheshimiwa Rais
1. Uhalali wa Kisheria wa Kampuni ya Acacia Mining Plc
nchini Tanzania.
Kamati imebaini na kuthibitisha kwa mujibu wa nyaraka na
maelezo kutoka ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA) kuwa
kampuniya Acacia Mining Plc haikusajiliwa (incorporation)
nchini Tanzania na wala haina hati ya utambuzi (certificate
of compliance) kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, Sura
ya 212.
Kamati pia imebaini kuwa kampuni ya Acacia Mining Plc,
ambayo inajinasibisha kuwa mmiliki wa makampuni ya
Bulyanhulu Gold Mines Ltd, North Mara Gold Mine Ltd na
Pangea Minerals Ltd, haikuwahi kuwasilisha nyaraka wala
taarifa yoyote kuonesha kuwa kampuni hiyo ni mmiliki wa
makampuni hayo wala kuwa na hisa katika makampuni
hayo. Kwa kuwa Acacia Mining Plc haina usajili wala
utambuzi wa kisheria nchini Tanzania, haina sifa ya kupata
9
leseni, kuchimba wala kufanya biashara ya madini nchini
Tanzania.
Hivyo basi, Kamati imebaini kuwa Acacia Mining Plc,
inafanya biashara ya madini hapa nchini kinyume cha
sheria za nchi.
2. Biashara ya Uuzaji na Usafirishaji wa Makinikia Nje ya
Nchi
Mheshimiwa Rais,
Kamati ilibaini kuwa makampuni ya Bulyanhulu Gold Mines
Ltd na Pangea Minerals Ltd ndizo wazalishaji na wauzaji wa
makinikia nje ya nchi. Kwa mujibu wa mikataba ya mauzo ya
makinikia baina ya makampuni hayo na wafanyabiashara
kutoka nje ya nchi, makinikia husafirishwa kutoka Tanzania
yakiwa yameshauzwa na hupelekwa nje ya nchi kwa madai
ya kwenda kuchenjuliwa kupitia Bandari za Dar es Salaam
na Tanga. Makinikia hayo hupelekwa nchi za China, Japani
na Ujerumani, yakiwa kwenye makontena yenye urefu wa
futi 20 na wastani wa tani 20 kila moja. Wafanya biashara
wa makinikia ni makampuni yaitwayo Aurubis AG na Aurubis
Bulgaria ADM, Mark Rich Co. Investment AG na Pan Pacific
Copper Co. Limited kutoka nchi za Ujerumani, Uswisi na
Australia. Mauzo hayo ya makininkia hufanywa kwa mujibu
wa mikataba ya uchimbaji wa madini kati ya Serikali na
Makampuni ya uchimbaji madini (Mining Development
10
Agreements-MDAs). Kutokana na taarifa za kiuchunguzi
(forensic investigation) kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) mauzo ya makininkia hufanyika kupitia Ofisi ya Uhasibu
(Treasury Department) ya makampuni hayo iliyopo Afrika ya
Kusini.
3. Utaratibu wa Uuzaji Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais,
Kamati imebaini kwamba kifungu cha 51 cha Sheria ya
Madini kinaruhusu mwenye leseni ya uchimbaji wa madini
kufanya biashara ya madini, ikiwa ni pamoja na kuuza nje ya
nchi. Kifungu hicho kinamtaka mwenye leseni ya uchimbaji
kupata kibali cha kusafirisha madini kutoka kwa Afisa
Mwenye Mamlaka atayethibitisha kwamba mrahaba stahiki
umelipwa kwa Serikali. Mbali ya kupata kibali kinachoonesha
malipo ya mrahaba hakuna utaratibu mwingine maalum
katika biashara ya uuzaji na usafirishaji wa makinikia nje ya
nchi. Aidha, kisheria makampuni ya madini yanapaswa
kutoa taarifa sahihi kwa Serikali kuhusu aina, kiasi na thamani
ya madini yaliyomo ili kuiwezesha Serikali kukokotoa na
kutoza mrahaba stahiki.
Mheshimiwa Rais,
Kwa kuzingatia nyaraka na taarifa mbalimbali za
kiuchunguzi, Kamati imeridhika kuwa baadhi ya watumishi
wa Serikali, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini,
11
makampuni ya usafirishaji na upimaji wa madini na
makampuni yenyewe yametenda makosa mbalimbali ya
kijinai yakiwemo ukwepaji wa kodi, kutoa taarifa za uwongo,
kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, uhujumu uchumi na
kulisababishia taifa hasara kinyume cha:
i. vifungu vya 18,114 na 115 vya Sheria ya Madini,
2010
ii. vifungu vya 101 na 106 vya sheria ya kodi ya
mapato, 2004
iii. vifungu vya 79 na 82 vya Sheria Usimamizi wa
kodi, 2015
iv. kifungu cha 24 cha Sheria ya Uwazi na uwajibikaji
katika sekta ya Madini Tanzania, 2015
v. Kifungu cha 27 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu
Uchumi sura ya 200, na
vi. Kifungu cha 203 cha Sheria ya Usimamizi wa
Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,2004
Kwa kuzingatia nyaraka na taarifa mbali mbali za
kiuchunguzi Kamati pia imeridhika kuwa baadhi ya
watumishi wa Serikali, watumishi na wamiliki wa makampuni
ya madini, makampuni ya usafirishaji na upimaji wa madini
na makampuni yenyewe wamelitia aibu Taifa kwa kutenda
makosa mbali mbali yakiwemo, ukwepaji wa kodi, kutoa
taarifa za uwongo, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu,
uhujumu uchumi na kulisababishia taifa hasara.
12
Mheshimiwa Rais,
Kamati pia imebaini kwamba, katika kufanya biashara ya
makinikia makampuni ya Bulyanhulu na Pangea yamekuwa
yakiuza makinikia nje ya nchi pasipo kufuata utaratibu kwa
namna ambayo vitendo vifuatavyo vimedhihirika:
i. Udanyanyifu wa kibiashara na ukwepaji wa kodi
ambao umesababisha:
a. Kuficha idadi, uzito na thamani ya madini
yaliyomo kwenye makontena 277 yaliyozuiwa
katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa kiwango
cha wastani kuonesha kwamba thamani yake ni
TZS 79,939,900,989.49 (TZS 79.94 bilioni), wakati
thamani halisi, kwa mujibu wa uchunguzi wa
kimaabara uliofanywa na Kamati Maalum Na. I,
unaonesha kuwa thamani halisi ya madini
yaliyomo, ni kati ya TZS 829,361,455,861 (TZS 829.36
bilioni) kwa kiwango cha chini, na TZS
1,438,760,551,512 (TZS 1.438 trilioni) kwa kiwango
cha juu.
b. Mgongano au kusigana kwa taarifa za uzito na
idadi ya makontena kati ya nyaraka za kusafirishia
makontena (kadhia) ukilinganisha na nyaraka za
wakala wa meli (shipping orders). Idadi na uzito
wa makontena ikiwa kubwa zaidi kwenye nyaraka
za wakala wa meli kuliko kadhia (export entry)
zilizotengenezwa na makampuni hayo kwa lengo
la kusafirishia makontena nje ya nchi.
13
c. Kiasi cha mrahaba kilichooneshwa katika vitabu
vya hesabu za makampuni ya Bulyanhulu na
Pangea zimeonesha kwamba, Dola za Marekani
111,304,561.00 (USD 111.3 milioni) zililipwa Serikalini
kama mrahaba kati ya mwaka 1998 na 2017,
lakini vitabu vya hesabu vilivyopo Wizara ya
Nishati na Madini zinaonesha malipo yalikuwa
Dola za Marekani 42,702,727.50 (USD 42.7 milioni).
Hali hii inaonesha upungufu wa kiasi cha Dola za
Marekani 68,601,833.50 (USD 68.6 milioni)
zilizopaswa kulipwa kama mrahaba.
d. Makampuni ya wakala wa meli ya Freight
Forwarders (T) Limited, Quick Services Clearing
and Forwarding Limited na Walford Meadows Co.
Ltd, ziliwasilisha nyaraka za uwongo za usafirishaji
wa makinikia kutoka Kahama Mining Corporation,
(baadaye Bulyanhulu Gold Mine Ltd) na Pangea
Minerals Ltd, katika kipindi cha kati ya mwaka
1998 na 2017.
e. Kutoa taarifa za uwongo za uchenjuaji nje ya nchi
wakati makanikia hayo yameuzwa kabla ya
kusafirishwa kutoka Tanzania kupelekwa nchi za
nje.
ii. Kufanya magendo katika biashara ya makinikia:
a. Makontena 30 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia
yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi
Na.1482 ya tarehe 23.7.2001. Hata hivyo,
14
iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na.
TZGT00000552 kuwa makontena 33 yenye urefu
wa futi 20 ndiyo yalisafirishwa na kwa sababu hiyo
yakionyesha makontena matatu zaidi ya idadi
iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji melini
iliyoandaliwa na wakala wa usafirirshaji, kwa
niaba ya makampuni ya uchimbaji madini.
b. Makontena 60 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia
yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi
Na. 1483 ya tarehe 7.8.2001. Hata hivyo,
iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na.
MOL-1 ya makontena hayo hayo, kuwa
makontena 67 yenye urefu wa futi 20 ndiyo
yalisafirishwa na kwa sababu hiyo, ikiwa ni
makontena saba (7) zaidi ya idadi iliyooneshwa
na wakala wa usafirishaji, kwa niaba ya
makampuni ya uchimbaji madini.
c. Makontena 48 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia
yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi
Na.1487 ya tarehe 27.8.2001. Hata hivyo,
iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na.
Mol-100038 kuwa makontena 67 yenye urefu wa
futi 20 yalisafirishwa na kwa sababu hiyo
yakionyesha makontena kumi na tisa (19) zaidi ya
idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji
melini iliyoandaliwa na wakala wa usafirirshaji kwa
niaba ya makampuni ya uchimbaji madini.
15
d. Makontena 85 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia
yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi
Na.1504 ya tarehe 20.12.2001. Hata hivyo,
iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na.
Mol-01 kuwa makontena 99 yenye urefu wa futi 20
ndiyo yalisafirishwa na kwa sababu hiyo
yakionesha makontena kumi na nne (14) zaidi ya
idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji
melini iliyoandaliwa na wakala wa usafirishaji, kwa
niaba ya makampuni ya uchimbaji madini.
iii. Ukwepaji wa kodi ya mapato kwa njia ya udanganyifu
wa bei ya bidhaa au huduma (transfer price
manipulation).
a. Mauzo ya makinikia kwa wafanyabiashara na
wachenjuaji nje ya nchi hayakufanyika kwa
ushindani kutokana na kuonesha vipindi virefu vya
uhusiano wa kibiashara kwa kuzingatia nyaraka za
mikataba baina yao.
b. Masharti ya usafirishaji wa makinikia ulionyeshwa
kuwa free on board (f.o.b) badala ya cost and
freight (c.fr) au cost, insurance and freight (c.i.f)
makanikia hayo yaliuzwa kwa wafanya biashara
wale wale na wachenjuaji wale wale wenye
16
mahusiano ya kibiashara kama ilivyooneshwa
katika mikataba ya mauzo ya makinikia baina
yao.
c. Madini yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa
makinikia hasa badala yake, yalikuwa ni madini
ya aina mbali mbali mahususi yaliyopatikana
kutokana na uchenjuaji kwa njia ya ‘carbon–inleach’
(CIL).
iv. Upandishaji wa gharama za uendeshaji migodi:
Uchunguzi wa kisayansi wa mifumo ya computa
(forensic examination kupitia TRA, umebaini kwamba
gharama za utafutaji na upembuzi wa miamba yenye
madini imejumuishwa kwenye gharama za mauzo na
kwa sababu hiyo, kuathiri faida halisi ambayo ilipaswa
kutozwa kodi. Hali hii imesababisha faida ya
makampuni kutoonekana na kwa sababu hiyo kuathiri
msingi wa ukokotoaji kodi ya mapato ya makampuni
(tax base for corporate tax).
v. Mrahaba ambao haukukusanywa
Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2007, 2011 na 2012
zilizotolewa na PriceWater Coopers, bei ya dhahabu
katika soko la kimataifa imekuwa ikipanda na
kuwezesha makampuni ya madini kupata faida zaidi
ya asilimia 1,400 mwaka 2002 na 2006 ambapo
17
Bulyanhulu na Pangea, zilipata faida ya asilimia 32.
Hata hivyo, faida yote iliyopatikana kutokana na
kupanda kwa bei ya dhahabu haikuoneshwa kwa
madhumuni ya malipo ya mrahaba kwa Serikali.
vi. Uhamishaji haramu wa fedha
Uchunguzi wa kisayansi na mifumo ya komputa kupitia
TRA imebainika kuwa faida iliyooneshwa na Kampuni
mama (Holding Company) iliyopo nje ya nchi ya
Tanzania imekuwa ikirudishwa kwenye makampuni ya
uchimbaji nchini kama mikopo iliyotolewa na riba zake.
Baadaye riba inayotozwa kwenye taarifa za hesabu
Kama gharama kwa makampuni ili kutumika katika
kukokotoa kodi ya mapato ya kampuni (Assessment of
Corporate Income Tax).
Thamani ya Madini Yalimo kwenye Makinikia Kwenye
Makontena 44,277
Mheshimiwa Rais,
Uchunguzi wa Kamati ulibaini kuwepo takwimu mbali mbali
za idadi ya makontena yaliyosafirishwa nje nchi kuanzia
mwaka 1998 hadi mwezi Machi 2017. Hata hivyo, Kamati
iliamua kutumia takwimu kutoka Idara ya Forodha na Ushuru
wa Bidhaa (TRA) kwa kuwa, moja ya majukumu ya idara
hiyo ni kukusanya takwimu za bidhaa zote zinazosafirishwa
nje ya nchi kupitia bandari, viwanja vya ndege na mipaka
18
ya nchi. Kutokana na chanzo hicho idadi ya makontena
yaliyosafirishwa yalikuwa 44,277 kwa kiwango cha chini na
makontena 61,320 kwa kiwango cha juu kutoka kwenye
vyanzo vyetu vya uchunguzi.
Viwango vya Dhahabu kwenye Makinikia
Mheshimiwa Rais,
Viwango vya dhahabu vilikuwa na wastani wa 28 kg za
dhahabu kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha
dhahabu kwenye kila kontena, makontena 44,277 yatakuwa
na dhahabu kiasi cha tani 1,240. Kiasi hiki kina thamani ya
TZS 108,062,091,984,000 (TZS 108.06 trilioni), sawa na USD
49,119,132,720 (USD 49.12 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha
juu cha dhahabu kwa kontena moja (47.5 kg), kiasi cha
dhahabu katika makontena 44,277 kitakuwa tani 2,103
ambazo thamani yake ni TZS 183,319,620,330,000 (TZS 183.32
trilioni), sawa na USD 83,327,100,150 (USD 83.32 bilioni).
Viwango vya Madini ya Silver, Copper, Sulphur, Iron, Nickel
na Zinc kwenye Makinikia
Madini ya Silver
Kiwango cha Silver kilikuwa ni wastani wa 6.1 kg kwa kila
kontena. Kwa kutumia kiwango hicho kwa kila kontena,
makontena 44,277 yatakuwa na Silver kiasi cha tani 270. Kiasi
hiki kina thamani ya TZS 329,660,684,232 (TZS 329.66 bilioni),
19
sawa na USD 149,845,766 (USD 149.8 milioni). Kwa kutumia
kiwango cha juu katika kontena moja (7 kg) kiasi cha Silver
katika makontena 44,277 kitakuwa tani 309 ambazo thamani
yake ni TZS 378,299,145,840 (TZS 378.3 bilioni) sawa na USD
171,954,157 (USD 172 milioni).
Madini ya Copper
Kiwango cha copper kilikuwa na wastani wa 5,200 kg
kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha copper
kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277
yatakuwa na copper kiasi cha tani 230,240. Kiasi hiki cha
copper kina thamani ya TZS 2,861,888,172,000 (TZS 2.86 trilioni)
sawa na USD 1,300,858,260 (USD 1.3 bilioni). Kwa kutumia
kiwango cha juu cha copper kwa kontena moja (6,756 kg),
kiasi cha copper katika makontena 44,277 kitakuwa tani
299,135 ambazo thamani yake ni TZS 3,718,253,171,160 (TZS
3.72 trilioni) sawa na USD 1,690,115,078 (USD 1.692 bilioni)).
Madini ya Sulphur
Kiasi cha Sulphur kilikuwa na wastani wa 7,800 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha Sulphur kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na
Sulphur kiasi cha tani 345,360. Kiasi hiki cha Sulphur kina
thamani ya TZS 227,937,996,000 (USD 103,608,180). Kwa
kutumia kiwango cha juu cha sulphur kwa kontena moja
lenye uzito wa 10,160 kg, kiasi cha Sulphur katika makontena
44,277 kitakuwa tani 449,854 ambazo thamani yake ni TZS
20
296,903,851,200 (TZS 296.9 bilioni), sawa na USD 134,956,296
(USD134.96 milioni).
Madini ya Iron
Kiwango cha iron kilikuwa na wastani wa 5,400 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha iron kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na iron
kiasi cha tani 239,095. Kiasi hiki cha iron kina thamani ya TZS
368,207,532,000 (USD 167,367,060). Kwa kutumia kiwango
cha juu cha iron kwa kontena moja lenye uzito wa 6,100 kg,
kiasi cha iron katika makontena 44,277 kitakuwa tani 270,089
ambazo thamani yakeni ni TZS 415,938,138,000 (TZS 415.94
bilioni), sawa na USD 189,062,790 (USD 189.06 milioni).
Madini ya Nickel na Zinc
Zinc
Kiwango cha zinc kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha zinc kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na zinc
kiasi cha tani 1,474. Kiasi hiki cha zinc kina thamani ya TZS
8,433,705,852 (TZS 8.43 bilioni) sawa na USD 3,833,503 (USD
3.83 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa
kwa makontena moja (65.8 kg) kiasi cha zinc katika
makontena 44,277 kitakuwa na uzito wa tani 2,913 kg
ambazo thamani yake ni TZS 16,664,800,152 (TZS16.66 bilioni),
sawa na USD 7,574,909 (USD 7.57 milioni).
21
Nickel
Kiwango cha nickel kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha nickel kwenye kila
makontena, makontena 44,277 yatakuwa na nickel kiasi cha
tani 620. Kiasi hiki cha nickel kina thamani ya TZS
13,228,196,520 (6,012,817). Kwa kutumia kiwango cha juu
kilichopimwa kwa makontena moja kiasi cha inickel katika
makontena 44,277 kitakuwa tani 1,771 ambazo thamani
yakeni ni TZS 37,794,847,200 (USD 17,179,476).
Madini ya kundi la Platinum
Rhodium
Viwango vya rhodium vilikuwa na wastani wa 0.034 kg za
rhodium kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha
rhodium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na rhodium kiasi cha tani 1.5. Kiasi hiki cha
rhodium kina thamani ya TZS 105,754,560,707 (TZS 105.75
bilioni), sawa na USD 6,012,817 (USD 6.01 milioni). Kwa
kutumia kiwango cha juu cha rhodium kwa kontena moja
0.078 kg, kiasi cha rhodium katika makontena 44,277
kitakuwa tani 3.5 kg ambazo thamani yake ni TZS
242,613,403,976 (TZS 242.6 bilioni), sawa na USD 110,278,820
(USD 110.28 milioni).
22
Iridium
Kiwango cha iridium kilikuwa ni wastani wa 6.4 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha iridium kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na
iridium kiasi cha tani 283. Kiasi hiki cha iridium kina thamani
ya TZS 17,187,693,811,200 (TZS 17.19 trilioni), sawa na USD
7,812,588,096 (USD1.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu
iridium kwa makontena moja 13.75 kg, kiasi cha iridium
katika makontena 44,277 kitakuwa tani 609 kg ambazo
thamani yake ni TZS 36,926,685,922,500 (TZS 36.93 trilioni),
sawa na USD 16,784,857,238 (USD 16.9 bilioni).
Viwango vya Metali za Rare Earth Elements (REE), Transition
Elements na Light Elements
Ytterbium
Kiwango cha ytterbium kilikuwa ni wastani wa 3.7 kg za
ytterbium kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha
ytterbium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena
44,277 yatakuwa na ytterbium kiasi cha tani 164. Kiasi hiki
cha ytterbium kina thamani ya TZS 1,982,281,290,000 (TZS 1.98
trilioni), sawa na USD 901,036,950 (USD 901 milioni). Kwa
kutumia kiwango cha juu ytterbium kwa kontena moja 4.9
kg, kiasi cha ytterbium katika makontena 44,277 kitakuwa
tani 217 kg ambazo thamani yake ni TZS 2,625,183,330,000
(TZS 2.63 trilioni), sawa na USD 1,193,265,150 (USD 1.2 bilion).
23
Beryllium
Kiwango cha beryllium kilikuwa wastani wa 19.4 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha beryllium kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na
beryllium kiasi cha tani 859. Kiasi hiki cha beryllium kina
thamani ya TZS 956,209,634,160 (TZS 956.2 bilioni), sawa na
USD 434,640,743 (USD 434.64 milioni). Kwa kutumia kiwango
cha juu cha beyllium kwa kontena moja 26.9 kg kiasi cha
beryllium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,310 kg
ambazo thamani yake ni TZS 1,325,878,307,160 (TZS1.32
trilioni), sawa na USD 602,671,958 (USD 602.67 milioni).
Tantalum
Kiwango cha tantalum kilikuwa ni wastani wa 11.7 kg
kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha tantalum
kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277
yatakuwa na tantalum kiasi cha tani 518. Kiasi hiki cha
tantalum kina thamani ya TZS 300,878,154,720 (TZS 300.87
bilioni), sawa na USD 136,762,798 (USD 136.76 milioni). Kwa
kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwa kontena moja
(17.3 kg), kiasi cha tantalum katika makontena 44,277
kitakuwa tani 766 kg ambazo thamani yake ni TZS
444,888,211,680 (TZS 444,88 bilioni), sawa na USD 202,221,914
(USD 202.2 milioni).
24
Lithium
Kiwango cha lithium kilikuwa wastani wa 21.5 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha lithium kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na
lithium kiasi cha tani 952. Kiasi hiki cha lithium kina thamani
ya TZS 164,821,575,270 (TZS 164.82 bilioni), sawa na USD
74,918,898 (USD 74.91 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu
lithium kwa kila kontena moja lenye 29.8 kg, kiasi cha lithium
katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,319 ambazo
thamani yake ni TZS 228,450,369,444 (TZS 228.4 bilioni), sawa
na USD 103,841,077 (USD 103.84).
Mheshimiwa Rais,
Jumla ya thamani ya madini katika makontena 44,077
yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi cha mwaka 1998
hadi 2017 kwa kutumia kiwanjumla ya thamani ya madini
katika makontena 44,077 kwa kutumia kiwango cha wastani
ni TZS 132,569,087,296,991 (TZS 132.56 trilioni) sawa na USD
60,258,676,044 (USD 60.25 bilioni) au TZS 229,977,173,828,312
(TZS 229.9 trilioni) sawa na USD 104,535,079,013 (USD 104.5
bilioni.) kwa kiwango cha juu.
25
Thamani ya Madini Yaliyomo kwenye Makinikia Kwenye
Makontena 61,320
Viwango vya Dhahabu
Kiwango cha dhahabu kwenye makinikia kilikuwa ni wastani
wa 28 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha
dhahabu kwenye kila kontena la tani 20, makontena 61,320
yatakuwa na dhahabu kiasi cha tani 1,717. Kiasi hiki cha
dhahabu kina thamani ya TZS 149,657,101,440,000 (TZS 149.65
trilioni), au USD 68,025,955,200 (TZS 68 bilioni). Kwa kutumia
kiwango cha juu cha dhahabu kwa kontena moja kwa uzito
wa 47.5 kg, kiasi cha dhahabu katika makontena 61,320
kitakuwa tani 2,913 ambazo thamani yake ni TZS
253,882,582,800,000 (TZS 253.8 trilioni), sawa na USD
115,401,174,000 (USD 115 bilioni).
Viwango vya Madini ya Silver, Copper, Sulphur, Iron, Nickel
na Zinc kwenye Makinikia
Madini ya Silver
Kiwango cha Silver kilikuwa wastani wa 6.1 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha silver kwenye kila
makontena la uzito wa tani 20, makontena 61,320 yatakuwa
na Silver kiasi cha tani 20. Kiasi hiki cha Silver kina thamani ya
TZS 456,552,909,120 (TZS 456.55 bilioni) sawa na USD
207,524,050 (USD207.5 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu
cha silver kwa kontena moja, 7 kg kiasi cha Silver katika
26
makontena 61,320 kitakuwa tani 429 ambazo thamani yake
ni TZS 523,913,174,400 (TZS 523.9 bilioni), sawa na USD
238,142,352 (USD 238.1 milioni).
Madini ya Copper
Kiwango cha copper kilikuwa wastani wa 5,200 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha copper kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na
copper kiasi cha tani 318,864. Kiasi hiki cha copper kina
thamani ya TZS 3,963,479,520,000 (TZS 3.9 trilioni), sawa na
USD 1,801,581,600 (USD 1.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha
juu copper kwa kontena moja (6,756 kg) kiasi cha copper
katika makontena 61,320 kitakuwa tani 414,278 ambazo
thamani yakeni ni TZS 3,718,253,171,160 (TZS 3.7 trilioni), sawa
na USD 1,690,115,078 (USD 1.6 bilioni).
Madini ya Sulphur
Kiwango cha Sulphur kilikuwa wastani wa 7,800 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena
lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na Sulphur kiasi
cha tani 478,296. Kiasi hiki cha Sulphur kina thamani ya TZS
411,187,392,000 (TZS 411.18 bilioni) sawa na USD 186,903,360
(USD 186.9 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu sulphur
katika kontena moja lenye uzito wa 10,160 kg, kiasi cha
Sulphur katika makontena 61,320 kitakuwa tani 623,011
ambazo thamani yake ni TZS 351,675,360,000 (TZS 351.67
bilioni) sawa na USD 143,488,000 (USD 143.5 milioni).
27
Madini ya Iron
Kiwango cha iron kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha iron kwenye kila
kontena, makontena 61,320 yatakuwa na iron kiasi cha tani
331,128. Kiasi hiki cha iron kina thamani ya TZS
509,937,120,000 (TZS 509 bilioni), sawa na USD 231,789,600
(USD231 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha iron kwa
kontena moja (6,100 kg) kiasi cha iron katika makontena
61,320 kitakuwa tani 374,052 ambazo thamani yake ni TZS
576,040,080,000 (TZS 576 bilioni) sawa na USD 261,836,400
(USD261 milion).
Madini ya Nickel na Zinc
Zinc
Kiwango cha zinc kilikuwa wastani wa 33.3 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye
tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na iron kiasi cha tani
2,042. Kiasi hiki cha zinc kina thamani ya TZS 11,679,988,320
(TZS 11.6 bilion) sawa na USD 5,309,086 (USD5.3 milioni). Kwa
kutumia kiwango cha juu cha zinc kwa kontena moja (65.8
kg) kiasi cha zinc katika kontena 61,320 kitakuwa tani 4,035
kg ambazo thamani yakeni ni TZS 23,079,376,320 (TZS 23.1
bilioni), sawa na USD 10,490,626 (USD 10 milioni).
28
Nickel
Kiwango cha nickel kilikuwa ni wastani wa 14 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye
tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na nickel kiasi cha tani
858. Kiasi hiki cha nickel kina thamani ya TZS 18,319,963,200
(TZS 18.3 bilioni), sawa na USD 8,327,256 (USD 8.3 milioni). Kwa
kutumia kiwango cha juu cha nickel kwa kontena moja 40
kg kiasi cha inickel katika kontena 61,320 kitakuwa tani 2,453
ambazo thamani yakeni ni TZS 52,342,752,000 (TZS 52 bilioni),
sawa na USD 23,792,160 (USD 23.7 milioni).
Madini ya kundi la Platinum
Rhodium
Kiwango cha rhodium kilikuwa na wastani wa 0.034 kg
kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha rhodium
kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320
yatakuwa na rhodium kiasi cha tani 2.5. Kiasi hiki cha
rhodium kina thamani ya TZS 146,461,360,584 (TZS 146 bilioni),
sawa na USD 66,573,346 (USD 66.5 milioni). Kwa kutumia
kiwango cha juu cha rhodium kwa kontena moja 0.078 kg
kiasi cha rhodium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 4.8 kg
ambazo thamani yake ni TZS 335,999,591,928 (TZS335.9
bilioni), sawa na USD 152,727,087 (USD 152.7).
Iridium
Kiwango cha iridium kilikuwa ni wastani wa 6.4 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena
29
lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na iridium kiasi
cha tani 392. Kiasi hiki cha iridium kina thamani ya TZS
23,803,540,992,000 (TZS 23.8 trilioni), sawa na USD
10,819,791,360 (USD 10.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha
juu cha iridium kwa kontena moja 13.75 kg kiasi cha iridium
katika kontena 61,320 kitakuwa tani 843 kg ambazo thamani
yake ni TZS 51,140,420,100,000 (TZS 51.1 trilioni), sawa na USD
23,245,645,500 (USD 23.2).
Viwango vya Metali za Rare Earth Elements (REE), Transition
Elements na Light Elements
Ytterbium
Kiwango cha tterbium kilikuwa wastani wa 3.7 kg kwenye kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha ytterbium kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na
ytterbium kiasi cha tani 227. Kiasi hiki cha ytterbium kina
thamani ya TZS 2,745,296,400,000 (TZS 2.7 trilioni), sawa na
USD 1,247,862,000 (USD1.24 milioni). Kwa kutumia kiwango
cha juu cha ytterbium kwa kontena moja 4.9 kg kiasi cha
ytterbium katika kontena 301 kitakuwa tani 217 kg ambazo
thamani yake ni TZS 3,635,662,800,000 (TZS 3.6 trilioni), sawa
na USD 1,652,574,000 (USD 1.6 bilioni).
Beryllium
Kiwango cha beryllium kilikuwa wastani wa 19.4 kg kwenye
kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena
30
lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na beryllium kiasi
cha tani 1,190. Kiasi hiki cha beryllium kina thamani ya TZS
1,324,271625,600 (TZS 1.3 trilioni), sawa na USD 601,941,648
(USD 601.9 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha
beryllium kwa kontena moja 26.9 kg kiasi cha beryllium katika
kontena 61,320 kitakuwa tani 1,650 kg ambazo thamani
yake ni TZS 1,836,232,305,600 (TZS 1.8 trilioni), sawa na USD
834,651,048 (USD 834.6 milioni).
Tantalum
Kiwango cha tantalum kilikuwa wastani wa 11.7 kg kwenye
kila kontena lenye tani 20, Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila
kontena, makontena 61,320 yatakuwa na tantalum kiasi cha
tani 717. Kiasi hiki cha tantalum kina thamani ya TZS
416,691,475,200 (TZS 416.6 bilioni), sawa na USD 189,405,216
(USD 189 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha
tantalum kwa kontena moja 17.3 kg kiasi cha tantalum
katika kontena 61,320 kitakuwa tani 1,061 kg ambazo
thamani yake ni TZS 616,133,548,800 (TZS 616.1 bilioni), sawa
na USD 280,060,704 (USD 280 milioni).
Lithium
Kiwango cha lithium kilikuwa na wastani wa 21.5 kg kila
kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha lithium kwenye kila
kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na
lithium kiasi cha tani 1,318. Kiasi hiki kina thamani ya TZS
228,264,313,200 (TZS 228.26 bilioni) sawa na USD 103,756,506
(USD 103.76 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha
31
lithium kwa kontena moja 29.8 kg, kiasi cha lithium katika
kontena 61,320 kitakuwa tani 1,827 ambazo thamani yake ni
TZS 316,384,955,040 ( TZS 316.38 bilioni) sawa na USD
143,811,343 (USD 143.81 milioni).
Mheshimiwa Rais
Thamani ya madini yote katika makontena 61,320
yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi kati ya 1998 na 2017
kwa kutumia kiwango cha wastani ni TZS 183,597,272,467,224
(TZS 183.597 trilioni) sawa na USD 83,453,305,667 (USD 83.45
bilioni). Jumla ya thamani ya madini katika makontena
61,320 yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi kati ya 1998
na 2017, kwa kutumia kiwango cha juu ni TZS
380,499,453,421,688 (380.499 trilioni) sawa na USD
144,772,478,828 (USD 144.77 bilioni).
Kiasi cha Mapato ambacho Tanzania Imepoteza (Kiwango
cha Chini)
Chanzo Kiasi (TZS)
kodi ya mapato ya makampuni 55,677,352,653,559
Kodi ya zuio la kodi 94,442,735,380
Mrahaba 11,147,480,869,759
Gharama za meli kutia nanga na
upakuaji
1,671,281,263,923
Jumla 68,590,557,522,621
32
Jumla ya mapato ya Serikali ambayo Serikali ilipoteza ni TZS
trillion 68.59 ambazo ni sawa na bajeti ya miaka miwili ya
Serikali kwa kigezo cha makadirio ya mwaka 2017/2018.
Aidha, robo ya fedha hizo zingetosha kujenga reli ya
Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
Kiasi cha Mapato ambacho Tanzania imepoteza (Kiwango
cha Juu)
Chanzo Kiasi (TZS)
Kodi ya mapato ya makampuni 95,548,006,939,893
Kodi ya zuio la kodi 94,442,735,380
Mrahaba 11,147,480,869,759
Gharama za meli kutia nanga na
upakuaji
1,671,281,263,923
Jumla 108,461,211,808,955
33
Jumla ya mapato ya ambayo Serikali ilipoteza ni TZS trilion
108.46, ambazo ni sawa na bajeti inayokaribia Miaka Mitatu
ya Serikali kwa kigezo cha Makadirio ya Matumizi ya mwaka
2017/2018 na gharama ya kujenga reli ya Standard Gauge
kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
4. Taarifa za Uchenjuaji Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais
Kamati imepata na kusom mikataba ya mauzo ya makinikia
kati ya makampuni ya uchimbaji na wachenjuaji. Katika
mikataba hiyo, Serikali siyo sehemu ya mikataba hiyo icha ya
kuwepo na salio la kodi katika makinikia hayo.
Aidha, mikataba hiyo haina masharti yanayozilazimu
kampuni za uchenjuaji kutoa taarifa za uchenjuaji kwa
Serikali au muuzaji.
34
Kwa msingi huo, taarifa ambazo zimekuwa zikiwasilishwa
kwa TMAA baada ya kuomba taarifa hizo kutoka
makampuni ya madini hazina ukweli na hazibebi takwimu
sahihi kuhusu aina, kiasi na thamani ya madini
yaliyochenjuliwa ambazo zingewezesha TRA kutoza kodi
stahiki.
5. Mikataba ya uchimbaji madini (Mining Development
Agreements-MDAs)
Mheshimiwa Rais,
Mikataba ya uchimbaji wa madini inafanyika chini ya
kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini, Sura 123. Kwa
mikataba iliyoingiwa mwaka 1994, mikataba hiyo ilifanyika
chini ya kifungu cha kifungu 15 cha Sheria ya Madini ya
Mwaka 1979 na kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini ya
Mwaka 1998 .
Mikataba mikubwa ya madini ni kama ifuatavyo:
i. Mgodi wa Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Kahama Mine
Corporation Limited).
Katika mkataba huu, Waziri wa Nishati na madini kwa
jitihada kubwa alifanikiwa kujadiliana na kampuni hii na
kuiwezesha Serikali kupata asilimia 15 za hisa katika
35
kampuni za uchimbaji Hata hivyo, mkataba huo
ulifanyiwa marekebisho mwezi Juni, 1999 na kusainiwa
na Waziri wa Nishati na Madini aliyefuata, Mheshimiwa
Dkt. Abdallah Omari Kigoda. Marekebisho hayo
yaliondoa asilimia 10 ya hisa ambazo Serkali ilikuwa
inamiliki na kubakiza asilimia 5 tu. Marekebisho
mengine katika mkataba huo huo yalifanyika Oktoba,
1999, ikiwa ni miezi minne tu tangu marekebisho ya
awali yafanyike. Marekebisho haya ya pili pia yalitiwa
saini na Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda ,
ambayo yaliondoa asilimia 5 ya hisa za Serikali
zilizokuwa zimebakia na hivyo, Serikali kubaki bila hisa
yoyote. Katika marekebisho hayo, Serikali ilikubali
kulipwa USD 5,000,000 ikiwa ni malipo ya mauzo ya hisa
za Serikali.
Aidha, Serikali ilikubali kuendelea kulipwa kiasi cha USD
100,000 kwa kila mwaka. Hata hivyo, Kamati haikuweza
kupata uthibitisho wa kufanyika kwa malipo ya jumla
ya USD 6,800,000.
Kamati imeona kwamba marekebisho hayo ya
mkataba yaliyofanywa na Mheshimiwa Dkt. Abdallah
Kigoda hayakuwa na maslahi kwa taifa kwani Serikali
ilipoteza haki ya umiliki wa hisa na kuinyima mapato
kutokana na gawio (dividend).
36
ii. Pangea Gold Mine Ltd
Kampuni hii ina mikataba miwili ya uchimbaji madini.
Mikataba wa kwanza ulisainiwa Disemba 2003 na
Mheshimiwa Daniel N.Yona akiwa Waziri wa Nishati na
Madini. Mkataba wa pili ulisainiwa na Mheshimiwa
Nazir M. Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na
Madini.Katika mikataba hii yote Serikali haina hisa
yoyote katika kampuni na pia mkataba huu unatoa
nafuu kubwa sana za kodi kwa kampuni, jambo
ambalo lina ikosesha Serikali kodi nyingi na mapato.
iii. North Mara Gold Mine Ltd ,
Mkataba huo ulisainiwa Juni 1999 na Mheshimwa
Daniel N.Yona, akiwa Waziri wa Nishati na Madini na
baadaye, marekebisho ya mkataba huo yalifanywa
mwaka 2007 na Mheshimiwa Nazir M. Karamagi akiwa
Waziri wa Nishati na Madini. Katika mkataba huo
Serikali haina hisa yoyote katika kampuni. Aidha katika
mkataba wa awali, uliotiwa saini na Mheshimiwa Daniel
N. Yona, Serkali ilitoa nafuu ya asilimia 15 ya nyongeza
ya mtaji wa kampuni (additional capital allowance),
na kuifanya kampuni hiyo iwe inajilipa kwanza ili
kurudisha mtaji wake na asilimia 15 iliyopewa na Serikali
na hivyo kusababisha kampuni kutangaza hasara
katika biashara kila mwaka. Jambo hilo limekuwa
linaikosesha Serikali kodi ya mapato. Kamati imebaini
kwamba marekebisho yaliyofanyika mwaka 2007
37
kuondoa nafuu ya asilimia 15, bado malimbikizo ya
hasara kutokana na nafuu ya kodi iliyokuwa imetolewa
na Serikali iliendelea kudaiwa na kampuni hii.
iv. Geita Gold Mine Ltd (AngloGold Ashanti Ltd);
Mkataba huu ulisainiwa na mheshimwa Dkt. Abdallah
Omari Kigoda akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Katika
mkataba huu Serikali haikupata hisa yoyote katika
kampuni na pia mkataba huu unatoa nafuu mbali
mbali za kodi kwa kampuni, jambo ambalo lina
ikosesha Serikali kodi nyingi na mapato.
Mikataba ya uchimbaji madini inaeleza kuwa
inaongeza na kurekebisha masharti yaliyomo katika
leseni za uchimbaji madini. Kamati inaona kuwa
masharti ya aina hiyo ni batili kisheria kwani Waziri
hawezi kurekebisha masharti ya leseni yaliyotolewa
kwa mujibu wa Sheria na Kanuni kwa kupitia vifungu
vya mkataba wa uchimbaji wa madini.
Aidha, Kamati imebaini kuwa kumekuwa na uongezaji
wa muda wa leseni (renewal) wa maeneo ya
uchimbaji madini kinyume cha sheria na bila
kuzingatia maslahi ya taifa.Kwa mfano, kuongeza
muda wa leseni na maeneo ya uchimbaji uliofanywa
na Mheshimiwa William M. Ngeleja na Mheshimiwa
Sospeter M. Muhongo, kwa kampuni za North Mara
Gold Mines limited na Pangea Minerals Limited.Pia
38
leseni mbali mbali zilizotolewa na; Kamishna Paulo M.
Masanja, Kamishna Dalaly P. Kafumu na Kaimu
Kamishna Ally B. Samaje. Katika kipindi hicho washauri
wakuu wa Serkali kwa masuala ya kisheria ni pamoja
na Mheshimiwa Andrew Chenge, Johnson Mwanyika
na Manaibu Wanasheria Wakuu ambao ni Felix Mrema
na Sazi Salula na Wakuu wa Idara ya Mikaba Maria
Ndossi Kejo na Julius Malaba.
b. Kifungu thabiti (stability clause)
Mikataba ya uchimbaji madini ina vifungu dhabiti
ambavyo vinazuia marekebisho ya sera na sheria
kuathiri masharti yaliyomo katika mikataba ya
uchimbaji madini. Kamati iliona kuwa pamoja na
uwepo wa vifungu thabiti, Serikali haizuiliwi kurekebisha
au kubadili Sera na Sheria zinazoweza kuathiri mikataba
ya uchimbaji madini. Aidha, mkataba wowote ule
hauwezi kisheria kuwa juu ya Mamlaka asili ya Nchi
(state soveregnity) na maslahi ya umma kuhusu
raslimali zake za asili.
Pia, mikataba hiyo ina vifungu vinavyoruhusu Serikali na
makampuni ya uchimbaji kujadili na kurekebisha sharti
lolote la kimikataba. Hivyo, mikataba ya uchimbaji
madini inaweza kurekebishwa. Ipo mifano mingi
inayoonesha kuwa masharti yenye vifungu dhabiti
haiondoi mamlaka ya nchi kufanya maamuzi ya kisera
39
au sheria ambayo yana maslahi kwa taifa na
wananchi wake. Kila nchi inayo kusimamia kanuni ya
umiliki wa milele wa mali asili yake kwa mujibu wa
azimio Na. 1803 la mwaka 1962 la Baraza kuu la Umoja
wa mataifa, Azimio Na. 3281 la 1974 la Baraza kuu la
Umoja wa Mataifa la Haki na Majukumu ya Kiuchumi
ya Mataifa. Maazimio yote yanatamka bila shaka haki
na mamlaka ya nchi kuweka mifumo ya kuondoa
unyonyaji katika maliasili na kuamua migogoro juu ya
mali asili ikiwemo madini, gesi na mafuta.
c. Misamaha ya kodi
Mikataba ya uchimbaji madini ina vifungu vingi
vinavyotoa misamaha mingi ya kodi ambayo haina
maslahi kwa taifa. Kwa kutumia mikataba hiyo,
makampuni yamekuwa hayalipi kodi kwa kutumia
kinga hiyo. Inatosha kusema kuwa mikataba hii haina
manufaa kwa Taifa.
d. Utunzaji na uhamishaji wa fedha katika mabenki
Mikataba ya uchimbaji madini inaruhusu kuweka na
kuhamisha fedha zinazotokana na mauzo ya madini
nje ya nchi. Kamati imeona kuwa hali hiyo inainyima
nchi nafasi ya kukuza uchumi, kuongeza thamani ya
fedha yake kutokana na mauzo ya madini kwa sababu
fedha haziwekwi katika mabenki yaliyomo ndani ya
nchi.
40
Aidha, kamati inaona kuwa utaratibu wa kuweka
fedha katika mabenki ya ndani ungewezesha
kupunguza mianya ya ukwepaji kodi unaofanywa na
makampuni ya madini. Ni wakati sasa nchi yetu
ikaachana na uhuru ambao makampuni ya migodi
yamepewa ya kuhifadhi fedha zitokanazo na madini
nje ya nchi. Ofisi za mauzo pia sharti ziwepo nchini na
siyo nje ya nchi.
e. Ajira na mafunzo kwa Watanzania
Mikataba ya uchimbaji madini ina zitaka kampuni za
madini kuajira kuwaendeleza wazawa kimafunzo ili
waweze kupata ujuzi na kuwa waendeshaji wakuu wa
shughuli za uchimbaji madini katika makampuni hayo
badala ya kuwaajiri watu wa nje.
Kamati imebaini kuwa hakuna utaratibu madhubuti
uliowekwa na Serikali katika kutimiza azma hiyo juu ya
mafunzo na ajira kwa wazawa. Kamati imeona
kwamba Tanzania inaweza kujifunza kutoka nchi ya
Ghana ambayo imeweka sharti la kuonyesha utaratibu
wa kipindi maalum cha mafunzo na ajira kwa wazawa
kama kigezo mojawapo muhimu kabla ya kampuni ya
uchimbaji madini kupewa leseni.
f. Uwajibikaji katika utoaji huduma kwa jamii
41
Mikataba ya uchimbaji madini inazitaka kampuni za
uchimbaji madini kushiriki na kuchangia kikamilifu
shughuli za maendeleo katika jamii inayowazunguka.
Kamati iliona taarifa za uchangiaji wa shughuli hizo za
maendeleo kwa jamii. Hata vivyo, uchangiaji huo ni
mdogo mno kulingana na mapato ya makampuni
hayo.
Kamati inaona ni vyema sheria ikaweka kiwango
maalum cha asilimia ya mapato inayotakiwa
kuchangiwa katika shughuli za maendeleo ya jamii.
6. Uhuru wa madaraka aliyo nayo Waziri (discretionary
powers)
Sheria ya Madini inatoa uhuru wa madaraka ya Waziri
katika kuingia katika mikataba ya madini na mambo
mengineyo. Kamati inaona kuwa madaraka hayo
yanapaswa kudhibitiwa na mikataba yote mikubwa ya
madinin inapaswa kupata idhini nya Bunge (ratified by
National Assembly/Parliament) kama nchi nyingine
kama Ghana inavyofanya.
7. Ushiriki wa Serikali katika uchimbaji wa madini
Kamati ilisoma sheria ya Madini na kuona kuwa haitoi
nafasi ya ushiriki wa Serikali katika umiliki wa hisa katika
makampuni ya uchimbaji madini. Kutokana na hali
42
hiyo kamati inaona kuna haja kuwa kifungu katika
Sheria ya madini kinachoweka kiwango maalum cha
asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na Serikali katika
makampuni yote ya madini nchini. Aidha Sheria itoe
hiari kwa Serikali kupata hisa nyingine kutoka kwa
makampuni ya madini nje ya asilimia itayowekwa na
Sheria kwa makubaliano na makampuni. Umiliki wa hisa
utaiwezesha Serikali kupata mapato na ushiriki katika
maamuzi muhimu katika biashara ya madini.
8. Kamati imeona hakuna sababu ya kupeleka migogoro
nje ya nchi kwa ajili ya usikilizwaji na uamuziikiwa wahisika
katika mikataba hiyo wote ni watanzania na migodi ipo
Tanzania. Aidha, kuna mahakama kuu ya Tanzania, kitengo
cha Biashara ambayo ipo kwa ajili ya migogogoro kama
hiyo. Kwa hiyo mahakama zetu zitumike kutatua migogoro
hiyo.
9. Kiwanda cha Uchenjuaji wa Makinikia
Tanzania inaweza kuanzisha na kuendesha kiwanda
cha kuchenjua makinikia kwa kuzingatia kuwa
teknolojia iliyopo ndani inayopatikana nje ya nchi
zinaweza zikatumika; mtaji unaweza kupatikana kwa
kutumia vyanzo vya ndani na mikopo; malighafi
inaweza kupatikana toka migodi ya ndani na kutoka
nchi jirani zinazochimba madini kama vile Zambia, na
Jamhuri ya Kidemikrasia ya Kongo.
43
10. Taasisi zenye Dhamana ya Kusimamia Sekta ya Madini
Tanzania ina taasisi nyingi zenye dhamana ya
kusimamia uendeshaji wa sekta ya madini pamoja na
ukadiriaji na ulipaji wa kodi za Serikali. Hata hivyo, kwa
bahati mbaya sana kwa muda mrefu Serikali imekuwa
ikipoteza mapato mengi sana kwenye sekta ya madini
kutokana na wizi na udanganyifu unaofanywa na
makampuni ya uchimbaji madini, watumishi wenye
tamaa na kujali masilahi binafsi na taasisi
zinazosimamia uendeshaji wa sekta ya madini
kushindwa kusimamia vyema sekta ya madini.
11. Ukosefu wa Wakala wa Meliwa Serikali
Mheshimiwa Rais
Nchi yetu imekuwa inapoteza mapato mengi sana
kupitia bandari zetu kwa kuwa Serikali haina wakala wa
meli ambaye angeweza kusimamia usafirishaji wa
mizigo nje kwa njia ya meli pamoja na biashara zingine
zote zinazohusiana na usafirishaji wa mizigo nje kwa
meli. Utaratibu huu ungeisaidia Serikali kwa kiwango
kikubwa kwa kuratibu na kuhakikisha mapato yote
yatokanayo na biashara hizi yanalipwa Serikali Kuu.
Sasa hivi, na hasa baada ya kuvunjwa kwa Wakala wa
Meli Tanzania (NASACO), biashara karibu zote
44
zinamilikiwa na kuendeshwa na wenye meli, ambao
wana ridhaa ya kupanga bei na hata kujilimbikizia
mapato ambayo yangestahili kwenda Serikalini.
Mapato mengi ya Serikali yanapotea kwa kutokuwa na
Wakala wa Meli wa Serikali; makadirio ya chini (kwa
makusudi) ya mirahaba; udanganyifu katika upimaji wa
kimaabara wa madini unaofanywa na TMAA na SGS;
Mapendekezo
Mheshimiwa Rais,
Kutokana na uchunguzi, Kamati Maalum imebaini kuwa
kuna ukiukwaji wa sheria za nchi na upotevu mkubwa wa
mapato ya Serikali kupitia biashara ya Makinikia na madini
yanayosafirishwa nje ya nchi. Kamati hii inatoa
mapendekezo kwa Serikali kama ifuatavyo:
1. Serikali, kupitia Msajili wa Makampuni ichukue hatua za
kisheria dhidi ya kampuni ya Acacia Mining Plc ambayo
imekuwa inaendesha shughuli zake nchini kinyume na
matakwa ya Sheria.
2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni
yote ya madini ambayo yamekwepa kulipa kodi na
mrahaba stahiki kwa mujibu wa sheria.
45
3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya
nchi mpaka hapo makampuni ya madini yanayodaiwa
yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki kwa mujibu
wa sheria.
4. Serikali ianzishe utaratibu utakowezesha ujenzi wa
kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia (smelter) ili
kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira
kwa watanzania.
5. Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria
dhidi ya waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa
Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za
mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa
Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa
Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia
mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za
uchimbaji wa madini na kuongeza muda wa leseni,
watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini,
makampuni yaliyohusika kuandaa nyaraka za usafirishaji
wa makinikia(Freight Forwarders(T)Ltd na makampuni ya
upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchina
upotoshaji.
6. Serikali ifute utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba
ya asilimia 90 na kusubiri malipo ya asilimia 10 kulipwa
46
baadaye wakati makampuni hayo ya madini huyauza
madini hayo na kupewa fedha taslimu kwa mkupuo.
7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa
Watumishi wa idara ya walipakodi wakubwa katika
Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kushughulikia
madai ya kodi ambayo Mabaraza ya Rufaani ya Kodi
na Mahakama zimekwisha yatolea uamuzi na vilevile
ichunguze mienendo ya watumishi wa mabaraza ya
Kodi kwa kutotolea maamuzi ya kesi za kodi kwa muda
mrefu kuhusu mashauri yaliyochukua muda mrefu
kukamilika katika vyombo hivyo.
8. Benki Kuu ya Tanzania ifuatilie malipo ya fedha za
kigeni yanayotokana na mrahaba kwa mauzo ya
madini.
9. Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya
migodi na viwanja ndege vilivyopo vigodini ili kudhibiti
vitendo vya hujuma vinavyoweza kuwa vinafanywa na
makampuni ya migodi ikiwemo utoroshaji wa madini.
10. Sheria iongeze kiwango cha adhabu zilizoainishwa kwa
makosa ya ukiukwaji wa Sheria ya Madini na Sheria za
Kodi.
47
11. Serikali kupitia wataalum wabobezi katika majadiliano
na mikataba (expert in negotiation and contract)
wapitie mikataba yote mikubwa ya uchimbaji madini
ipitiwe (review) na kufanya majadiliano na makampuni
ya madini ili kuondoa misamaha yote ya kodi isiyokuwa
na tija kwa taifa na badala yake kuweka masharti
yenye tija kwa pande zote mbili kwa kuzingatia maslahi
ya nchi;
12. Sheria iweke kiwango maalum cha asilimia ya hisa
ambazo zitamilikiwa na Serikali katika makampuni yote
ya madini nchini. Aidha, Sheria ielekeze Serikali kufanya
majadilaino ili kuwezesha Serikali kununua hisa katika
makampuni ya uchimbaji madini ili kuiwezesha kupata
mapato zaidi na ushiriki katika maamuzi muhimu katika
biashara ya madini.
13. Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara ya
usafirishajibidhaa nje ya nchi kupitia bandari kama
ilivyokuwa kama lilivyokuwa shirika la NASACO ili
kudhibiti biashara haramu na kuondoa mianya ya
ukwepaji kodi.
14. Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali asili ya
watanzania na iwekwe chini ya udhamini na uangalizi
wa Rais kwa manufaa ya watanzania.
48
15. Sheria itamke bayana kuwa mikataba yoyote ya
uchimbaji mkubwa wa madini (Mining Development
Agreement) isiwe ya siri na lazima yaridhiwe na Bunge
kabla ya kuanza kutekelezwa.
16. Sheria itoe masharti ya wazi ya kuzingatiwana iondoe
uhuru wa mamlaka ya (discretionary powers) za Waziri
wa Nishati na Madini, kamishna wa madini na maafisa
madini wakanda katika utoaji wa leseni za uchimbaji
madini.
17. Sheria ya madini iweka masharti kwamba mwombaji wa
leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini lazima yaoneshe
mchanganuo wa kina kuhusu namna mafunzo
kwawazawa yatakavyotolewa kwa lengo la ajiri kama
wataalam na kuchukua nafasi za uendeshaji wa migodi
husika na kupunguza au kuondoa kabisa wataalam
kutoka nje ya nchi.
18. Sheria ielekeze makampuni ya madini kuweka fedha
zinazotokana na mauzo ya madini katika benki zilizopo
nchini ili kuimarisha uchumi wa nchi na kuondoa mianya
ya ukwepaji wa kodi na tozo mbalimbali.
19. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au kufuta na
kubadili kabisa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi ili
kuondoapamoja mambo mengine masharti yote
49
yasikuwa na manufaa kwa taifa ikiwa ni pamoja na
masharti yaliyomo kwenye kifungu thabiti (stability
provision).
20. Serikali igharimie nakutoa mafunzo kwa watumishi wa
Serikali ili kuwapatia uelewa na weledi katika nyanja ya
majadiliano na uendeshaji wa mashauri yatokanayo na
mikataba ikiwemo ya mikataba ya madini (skills in
negotiation and arbitration).
21. Serikali kupitia Kamishna wa Madini iwe inafanya ukaguzi
wa mara kwa mara kaw makampuni ya madini ili
kujihakikishia uzingatia au ukiukwaji wa Sheria na
taratibu za uendeshaji na kuchukua hatua ipasavyo.
Mheshimiwa Rais,
Kwa mara nyingine tena mimi binafsi na kwa niaba ya
wajumbe wa kamati maalum, nakushukuru kwa imani yako
kwetu.
Kwa heshima kubwa, naomba kuwasilisha.

Ad