Home » Uchaguzi » Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 43 kufanyika Novemba 26 mwaka huu

Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 43 kufanyika Novemba 26 mwaka huu

07 October 2017 | Uchaguzi

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.

Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.

Jaji Kaijage amesema tume imetangaza kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.

Jaji Kaijage ameainisha kwamba kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.

Amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.

“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe 26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.

Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.

Jaji Kaijage aliema Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.

Alitoa mwito kwa vyama vya Siasa na Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.

Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:

 

Na

MKOA

HALMASHAURI

KATA

1.

ARUSHA

Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

Musa

Halmashauri ya Jiji la Arusha

Muriet

Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Ambureni

Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Ngabobo

Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Maroroni

Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Leguruki

Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Makiba

Halmashauri ya Wilaya ya Monduli

Moita

2. 2

DAR ES SALAAM

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni

Mbweni

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

Kijichi

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Saranga

3.

DODOMA

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

Chipogolo

4.

GEITA

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale

Bukwimba

Halmashauri ya Wilaya ya Geita

Senga

5.

IRINGA

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa

Kitwiru

Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo

Kimala

6.

KILIMANJARO

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi

Bomambuzi

Halmashauri ya Wilaya ya Hai

Mnadani

Halmashauri ya Wilaya ya Hai

Machame Magharibi

Halmashauri ya Wilaya ya Hai

Weruweru

7.

LINDI

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

Chikonji

Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

Mnacho

8.

MANYARA

Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’

Nangwa

9.

MBEYA

Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

Ibighi

10.

MOROGORO

Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro

Kiloka

Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi

Sofi

11.

MTWARA

Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

Milongodi

Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani

Reli

Halmashauri ya Mji wa Masasi

Chanikanguo

12.

MWANZA

Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Kijima

Halmashauri ya Jiji la Mwanza

Mhandu

13.

RUKWA

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

Sumbawanga

14. 14

RUVUMA

Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Lukumbule

 
Ad