Home » Washirika » Nike yashinda kesi dhidi ya 'Viatu vya shetani' vyenye tone la damu ya binadamu

Nike yashinda kesi dhidi ya 'Viatu vya shetani' vyenye tone la damu ya binadamu

02 April 2021 | Washirika

 

 

Lil Nas X and MSCHF's Satan Shoes sold out in less than a minute on Monday

CHANZO CHA PICHA,MSCHF

Rapa Lil Nas X kwa ushirikiano na kampuni ya MSCHF iliuza viatu vyote ilivyotengeneza chini ya dakika moja Jumatatu

Kampuni maarufu kwa viatu vya michezo ya Nike imeshinda keshi dhidi ya kampuni ya MSCHF juu ya 'Viatu vya shetani' vilivyosababisha utata ambavyo zinasemekana kuwa na tone la damu ya binadamu kwenye soli yake.

Viatu hivyo vinavyouzwa kwa dola 1,018 sawa na (pauni 740), ambavyo vimechorwa alama ya msalaba iliyopinduliwa na pentagramu (nyota ya ncha tano katika duara) na maneno "Luka 10:18", vimetengenezwa kwa kuboresha muundo wa kiatu cha Nike Air Max 97s.

MSCHF ilitengeneza viatu hivyo kwa ushirikiano na mwanamuziki Lil Nas X.

Kampuni ya MSCHF ilisema kuwa ilitengeneza viatu 666 pekee na vyote tayari vishauzwa.

Kampuni ya Nike imedai kuwa MSCHF imetumia nembo yake ya kibiashara na kuomba mahakama kusitisha kampuni hiyo kuuza viatu hivyo na pia iizuie kutumia nembo yao ya muda mrefu maarufu kama 'Swoosh'.

"Kampuni ya MSCHF na viatu vyake vya shetani ambavyo havijaidhinishwa kuna uwezekano mkubwa kukasababisha mkanganyiko na dhana fulani na kutengeneza fikra mbaya kati ya bidhaa ya kampuni ya MSCHF na kampuni ya Nike," Kampuni hiyo ya utengenezaji viatu vya michezo imesema.

Akitoa uamuzi unaopendelea kampuni ya Nike, jaji alitoa agizo la kuzuia uuzaji wa viatu hivyo hapo jana Alhamisi.

MSCHF ilizindua viatu vya rangi nyeusi na nyekundu "vilivyotolewa" Jumatatu, ikiwa ni sambamba na uzinduzi wa nyimbo mpya ya mwanamuzi Lil Nas X ya Montero ya (Call Me By Your Name), ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa YouTube Ijumaa iliyopita.

Katika video ya muziki huo, mwanamuziki huyo wa rapa anateleza kwenye mlingoti kutoka peponi au mbinguni hadi jehanamu au motoni, akiwa amevaa viatu hivyo.

Taswira na hiyo na viatu ambavyo vimeandikwa andiko la Bibilia Luka 10:18 - "Akawaambia, 'Nilimuona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni'."

Kila kiatu kina soli maalum ya muundo wa kampuni ya Nike yenye sentimita za ujazo 60 za wino mwekundu na tone la damu ya binadamu, ambayo ilichangiwa na wanachama wa kampuni hiyo.

Katika kesi yake, kampuni ya Nike imesema kuwa haikuidhinisha utengezaji wa viatu hivyo vya shetani.

 
Satan Shoes

CHANZO CHA PICHA,MSCHF

'Viatu vya shetani'

"Tayari kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha mkanganyiko na dhana potofu sokoni, ikiwemo wito wa kutaka watu kususia bidhaa za kampuni ya Nike kufuatia uzinduzi wa viatu vya shetani vya kampuni ya MSCHF, ambavyo inaonekana kana kwamba kampuni ya Nike ndiyo ambayo imeidhinisha na kuruhusu utengenezaji wa bidhaa za hiyo," kampuni ya Nike ilisema.

Kesi pia ilirejelea ujumbe wa mtandao wa Twitter uliotumwa na mshawishi mkubwa wa viatu Ijumaa iliyopita, ambao ulianza kuarifu wateja wake kuhusu kuzinduliwa kwa viatu hivyo na kuvipa umaarufu zaidi wikendi iliyopita kwenye mtandao wa kijamii na hata vyombo vya habari vya Marekani.

Baadhi ya wenye msimamo mkali akiwemo gavana wa Dakota Kusini Kristi Noem, na wafuasi wengine wa kidini, wameshutumu viatu hivyo vyenye utata na kumkosoa rapa Lil Nas X na kampuni ya MSCHF kwenye mtandao wa Twitter.

Hata hivyo, Lil Nas X alimjibu gavana huyo pamoja na viongozi wa kidini kwenye mtandao wa Twitter, na Jumatatu katika mtandao huo, kulikuwa na vibonzo vya mzaha kwenye wasifu wake baada ya kampuni ya Nike kusema kwamba imechukua hatua ya kisheria.

 
McKenzi Norris

CHANZO CHA PICHA,BBC OS ON WORLD SERVICE RADIO

 

McKenzi Norris amekosoa kampuni ya Nike kwa hatua iliyochukua

McKenzi Norris kutoka South Carolina, aliyenunua viatu hivyo, amesema kesi iliyowasilishwa na Nike imevuruga mipangilio yake ya kuuza tena viatu hivyo kwa dola 2,500 katika mtandao wa eBay, ambao uliondoa tangazo lake la kuviuza.

"Kwa ujumla, nafikiria kesi iliyowasilishwa na kampuni ya Nike haina msingi wowote ukizingatia uharibifu ambao imesababisha kwa watu wa kawaida kama mimi ambao biashara yao ni kununua bidhaa na kuziuza tena kwa njia halali," amesema.

/BBC

Ad