Home » Washirika » Prince Philip ambaye ni mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza amefariki dunia leo Aprili 09, 2021 akiwa na umri wa miaka 99.

Prince Philip ambaye ni mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza amefariki dunia leo Aprili 09, 2021 akiwa na umri wa miaka 99.

09 April 2021 | Washirika
Prince Philip ambaye ni mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza amefariki dunia leo Aprili 09, 2021 akiwa na umri wa miaka 99.
 
Philip amefariki dunia majira ya asubuhi katika Kasri la Windsor.
 
Mwezi Machi mwaka huu, Philip alisumbuliwa na maradhi ya moyo na licha ya kuruhusiwa kutoka hospitali, hali yake haikuimarika na aliendelea na matibabu katika Hospitali ya Mtakatifu Bartholomew nchini Uingereza.
 
Philip alimuoa Malkia Elizabeth mwaka 1947, ikiwa ni miaka mitano kabla ya Elizabeth kutawazwa kuwa malkia.
Ameacha watoto wanne, wajukuu nane na vitukuu 10.
Ad