Home » Node

Rais Magufuli afungua barabara ya Kyaka - Bugene na Azungumza na wananchi wa Kyaka na Bukoba Mjini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Novemba, 2017 amefungua barabara ya lami ya Kyaka – Bugene Mkoani Kagera yenye urefu wa kilometa 59.1 iliyogharimu Shilingi Bilioni 81.597 fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo yenye urefu wa kilometa 183.1 ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda na Burundi.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VIWILI MKOANI MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Oktoba, 2017 amefungua kiwanda cha kuzalisha bidhaa za plastiki cha Victoria Moulders na kiwanda cha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceuticals Co. Ltd vilivyopo katika wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza.

Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 43 kufanyika Novemba 26 mwaka huu

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.

Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.

Rais John Magufuli ameivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni (KDA)

Rais John Magufuli ameivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni (KDA) na  sasa shughuli zake zinahamishiwa katika Manispaa ya Kigamboni.

Akizungumza leo Jumatano,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema ametumwa na Rais Magufuli kutangaza uamuzi huo.

"Kumekuwa na mgongano katika usimamizi wa ardhi kati ya KDA na Manispaa ya Kigamboni, Rais ameliona hilo na kuamua kuivunja mamlaka hiyo,"amesema.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS