Home » Node

Tume ya uchaguzi Kenya imejipanga upya kuharakisha ujumlishaji wa matokeo ya kura za urais

 

Ikiwa ni siku ya Tano sasa wakenya wakisubiri kwa hamu na ghamu kumjua rais wao mpya, Tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC imelazimika kubadili mpango wake wa kazi ilikuharakisha ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi wa urais mbali na kuhakiki stakabadhi zinazotoka katika maeneo yote nchini.

Mkutano wa Kawaida wa 42 wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17 & 18,2022 Jijini Kinshasa,nchini DRC

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha maandalizi ya Mkutano wa Kawaida wa 42 wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17 & 18,2022 Jijini Kinshasa,nchini DRC

WAZIRI JAFO AELEKEZA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UPANDAJI MITI TANZANIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhusisha masharti ya upandaji miti kwa vibali vya ujenzi.

Ametoa maelekezo hayo  Agosti 11, 2022 wakati akishiriki uzinduzi wa kampeni ya ‘STAMICO na Mazingira At 50’ iliyokwenda sambamba na zoezi la upandaji miti katika eneo la wazi Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wamehutubia jukwaa la Wafanyabiashara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wamehutubia jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Wafanyabiashara wa Kenya Jijini Nairobi na kuwahakikishia kuwa Serikali za nchi zote mbili zipo tayari kuwapa ushirikiano wowote watakaouhitaji katika kukuza biashara na uwekezaji katika nchi hizo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uganda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uganda na Kampuni za Uwekezaji katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Mhe. Rais Samia amekutana na Timu hii Ikulu jijini Dodoma

Chad: Rais Idriss Déby afariki dunia,

Kulingana na uthibitisho kutoka katika jeshi la kitaifa la Chad uliosomwa kwenye redio ya taifa, Rais mpya aliyechaguliwa tena Idriss Déby amekufa kwa majeraha aliyoyapata wakati akiamuru jeshi lake katika vita dhidi ya waasi kaskazini.

Katika mabadiliko ya haraka ya hatima, baada ya habari kuja kuwa rais mkongwe wa Chad, Idriss Déby alishinda muhula wa sita katika matokeo ya hivi karibuni  Jumatatu na alipata 79.3%, tangazo lililotangazwa kwenye redio ya kitaifa leo limetangaza kifo chake.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS