Home » Node

Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele ya uzinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando

Zaidi ya wananchi 1200 wa kata ya Kirando inayojumuisha vijiji vinne vya Mtakuja, Mpata, Kichangani na Kamwanda, Wilayani nkasi Mkoani Rukwa, wajitokeza katika kuhakikisha uchimbaji na uwekaji wa msingi wa kituo cha afya cha kirando unakamilika ili kuweza kuanza upanuzi na ujenzi wa kituo hicho kitakachohudumia kata zaidi ya nne katika tarafa ya Kirando.  

 

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kutatua tofauti ndogondogo

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kutatua tofauti ndogondogo zinazojitokeza katika biashara kati ya nchi hizi mbili.

Marais hao wametoa maagizo hayo leo asubuhi tarehe 23 Februari, 2018 walipokutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Munyonyo mjini Kampala muda mfupi kabla ya kuanza kwa vikao vya mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa. amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba

WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa. amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba cha Namera Group of Industries na JOC.
 
Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu. Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 

Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) na Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.

Uteuzi wa Dkt. Omari Rashid Nundu na Bw. Waziri Waziri Kindamba umeanza tarehe 01 Februari, 2018.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS