"Madaktari 258 ambao waliokuwa waende Kenya, sasa waajiriwe Tanzania " JPM
Mnamo tarehe 18 Machi 2017 Ujumbe wa Serikali ya Kenya ukiongozwa na Waziri wa Afya Dkt. Cleopa Mailu uliwasili nchini ambapo ulikutana na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dhumuni la mkutano huo ulikua kuomba kuajiri, kwa Mkataba, Madaktari wa Tanzania mia tano (500), ili kupunguza uhaba wa Madaktari nchini Kenya.
Mheshimiwa Rais JPM, alikubali ombi hilo.




















