Home » Node

Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.

 

Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa ya tarehe 09 Desemba, 2016 amewaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara .

Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa kwa pamoja na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ,Jeshi la Polisi,Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa.

Serikali yatoa Bilioni 40 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba

SH. BILIONI 40 ZIMEPELEKWA WIZARA YA AFYA KWA AJILI YA UNUNUZI WA DAWA NA VIFAA TIBA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia sasa, Serikali imekwishaipatia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sh. bilioni 40 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Amesema hatua hiyo inalenga kupunguza changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba iliyokuwa inazikabili hospitali mbalimbali nchini.

Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno amewasili hapa nchini kwa ziara kikazi ya siku 2

Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno leo tarehe 27 Novemba, 2016 majira ya alasiri amewasili hapa nchini kwa ziara kikazi ya siku 2.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Idriss Deby Itno akiwa na Mkewe Mama Hinda Deby amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kisha kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na wananchi.

Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 20 Novemba, 2016 amemteua Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bw. Charles E. Kichere anajaza nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA iliyokuwa wazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uteuzi huu umeanza mara moja.

 

 

Gerson Msigwa

Uteuzi wa wenyeviti wawili wa hifadhi za jamii na Mmoja wa Chuo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa wenyeviti wawili wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii na mmoja wa chuo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja walioteuliwa kuwa ni kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Alhaji Mussa Iyombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS