Home » Node

Mradi wa Kidijitali kwa Shule za Msingi

Makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan amezindua mradi wa Kidijitali kwa Shule za Msingi katika Manispaa ya Dodoma wenye zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane unaokusudiwa kunufaisha takriban shule hamsini.

Akizungumza baada ya kuuzindua mradi huo mjini Dodoma, ambapo jumla ya wanafunzi elfu tano watakabidhiwa Ipad, Makamu wa Rais amesema mradi huo utasaidia juhudi za serikali katika kasi yake ya kuendea uchumi wa viwanda.

Mabaki ya kumbe NALEDI yapatikana

Wanasayansi nchini AFRIKA KUSINI wamebaini mabaki ya mifupa ya kiumbe kinachofanana kwa kiasi kikubwa na binadamu, ambayo yalifukiwa chini ya ardhi miaka mingi iliyopita.

Mabaki ya kumbe hicho kilichopewa jina la NALEDI, yamepatikana karibu na Mji wa JOHANNESBURG.

Kiumbe hicho kina mikono na miguu kama ya binadamu, ingawa maungo yake ni makubwa.

Rais Dk. John Magufuli hakukiuka Katiba ya Tanzania

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema, Rais Dk. John Magufuli hakukiuka Katiba ya Tanzania kwa kuwateua wabunge wawili wanaume.

Mwakyembe amesema hayo leo, kutoa ufafanuzi, wakati akizungumza na Uhuru FM,  kuhusu baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuzua mjadala hususan katika mitandao ya kijamii, kwamba Rais Dk. Magufuli amevunja Katiba kwa uteuzi alioufanya hivi karibuni wa kuwateua Profesa Palamagamba Kabudi na Abdallah Bulembo kuwa wabunge.

RAIS wa Gambia Yahya Jammeh amekataa kuondoka madarakani

RAIS wa Gambia Yahya Jammeh amekataa kuondoka madarakani kutoa nafasi ya kuapishwa kwa Adama Barrow hata baada ya makataa aliyopewa na Senegal kumalizika.

Barrow alipangiwa kuapishwa kuwa rais mpya Alhamisi, na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wako tayari kuingilia kati.

Rais huyo mteule sasa ametangaza kwamba ataapishwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal mwendo wa saa 16:00 GMT (saa moja Afrika Mashariki).

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 17 Januari, 2017 amemteua Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania.

Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Mjini Dodoma

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Mjini Dodoma kutekeleza majukumu yake kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Sita wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 31 Januari 2017. Kufuatia ratiba hiyo ya shughuli za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wote tayari  wamewasili Mjini Dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Kamati.

Katika kipindi chote hiki cha vikao hivyo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati ni kama ifuatavyo:

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS