Home » Node

Rais Magufuli atengua uteuzi wa DED Mkinga aitwaye Emmanuel Mkumbo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga ajulikanae kwa jina la Emmanuel Mkumbo.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Emmanuel Mkumbo kuanzia leo tarehe 18 Oktoba, 2016.

Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga atakayejaza nafasi ya Emmanuel Mkumbo utafanywa baadaye.

 

 

Vladimir Poutine ameamua kuahirisha ziara yake jijini Paris

Rais wa Urusi Vladimir Poutine ameamua kuahirisha ziara yake jijini Paris nchini Ufaransa ambayo ilipangwa kufanyika Octoba 19 ambako alitarajiwa kuzungumza na mwenyeji wake Francois Hollande.

 

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Kremlin jijini Moscou Dmitri Peskov, ziara hiyo imeahirishwa kwa sasa, itafanyika pale tu rais wa Ufaransa Francois Hollande atapojiskia vizuri.

 

Serikali ya Burundi kujiondoa ICC

Serikali ya Burundi imewapiga marufuku wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa baada ya kuchapisha ripoti iliyoituhumu serikali kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Ripoti iliyotolewa na wachunguzi hao ilibainisha maelfu ya watu kuteswa, kunyanyaswa kingono au kutoweka wakati wa machafuko ya kisiasa yaliyotokea tangu Aprili mwaka jana.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametishia kuvunja upya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Ufaransa

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametishia kuvunja upya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Ufaransa Mbele ya Bunge Jumatatu Oktoba 10, katika hotuba ya ufunguzi wa mwaka wa mahakama.

 

Kauli yake inatokana na hatua ya majaji wa Ufaransa kutangaza kufungua uchunguzi kuhusu mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS