Home » Node

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange ameweka jiwe la msingi la jengo la (TPA)

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange ameweka jiwe la msingi la jengo la Kituo cha Pamoja cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambalo limejengwa kwa lengo la kuwaweka pamoja wadau wote wanaotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma na kupunguza gharama kwa watumiaji wa bandari hiyo.

Rais Dkt. Magufuli, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana tarehe 02 Oktoba, 2016.

huduma katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kuimarishwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuboresha upatikanaji wa huduma katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa kuhakikisha inakuwa na  dawa na vifaa tiba vya kutosha.

 

Ametoa agizo hilo (Jumamosi, Oktoba Mosi, 2016) wakati alipotembelea hospitali hiyo akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.

Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania (2015-2020)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za umma kuhakikisha zinasogeza huduma za kijamii karibu na wananchi ili wazipate kwa urahisi na kwa gharama nafuu.  

 

Ametoa wito huo  (Jumatano, Septemba 21, 2016) wakati akizindua Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania (2015-2020) na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania kwenye eneo inapojengwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa (CCM) Dkt. Magufuli, amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Gazeti la Uhuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Septemba, 2016 amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Gazeti la Uhuru zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS