Home » Node

Serikali imeuza TANI LAKI 1 kati ya tani laki mbili na nusu ilizonunua kutoka kwa wakulima kwenye Oparesheni Korosho.

Serikali imeuza TANI LAKI 1 kati ya tani laki mbili na nusu ilizonunua kutoka kwa wakulima kwenye Oparesheni Korosho.

Mnunuzi amekubali kununua tani zote hizo kwa bei ya  Tsh. 4,480 kwa kilo moja sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 410.

Kampuni iliyosaini mkataba wa kununua korosho ghafi imekubali kulipa ushuru na kuicha serikali ikikusanya faida ya Tsh. Bilioni 150 baada ya kununua kwa Tsh. 3,300 kwa kila kilo kutoka kwa wakulima.

Eneo la Ekari 109 kutumika kujenga hospitali ya Uhuru jijini Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019), Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya maeneo mengine.

 

Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea na kujionea maendeleo ya nyumba za makaazi ya Polisi Mfikiwa Chake Chake Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya Askari Polisi Mfikiwa Chake Chake Pemba.

Makamu wa Rais ambaye yupo Pemba kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ambapo jana tarehe 10 Januari 2019 aliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar eneo la Pagali Chake Chake Pemba.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS