Home » Node

Utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji utakaotekelezwa kwa muda wa miezi 42 kuanzia sasa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri Mhe. Dkt. Mustafa Madbouly  tarehe 12 Desemba, 2018 wameshuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji utakaotekelezwa kwa muda wa miezi 42 kuanzia sasa.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB) ameongoza ujumbe maalum wa Tanzania kwenye mkutano wa tatu wa Dunia wa Utalii na Utamaduni,

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB) ameongoza ujumbe maalum wa Tanzania kwenye mkutano wa tatu wa Dunia wa Utalii na Utamaduni, ambao ni mkutano wa juu zaidi wa sera za utalii unaofanyika kila mwaka.

Rasmi..Diamond Kumuoa Huyu!

PENZI ni kikohozi kulificha huwezi! Hicho ndicho kilichotokea kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye rasmi ametangaza kuwa mbioni kumuoa mrembo shombeshombe wa Mombasa nchini Kenya anayejulikana kwa jina la Tanasha Donna Barbieri Oketch a.k.a Zahara Zaire.  Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa juu ya ishu hiyo mapema wiki hii, Diamond alikiri kuwa kwenye uhusiano na Tanasha ambaye ni mtangazaji wa Redio NRG ya jijini Mombasa, Kenya.

Alphonse Charahani: Mhandisi wa MV Nyerere aokolewa akiwa hai siku tatu baadaye

Mhandisi wa kivuko cha MV Nyerere Alphonse Charahani ameokolewa leo alfajiri akiwa hai.

Kwa sasa Charahani anaendelea kupokea matibabu kutoka kituo cha afya cha Bwisya Ukara.

Kufikia sasa idadi ya miilio iliopatikana ni 211 huku zaidi ya milli 116 kati yao ikitambuliwa na ndugu zao kulingana na waziri wa uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.

MV Nyerere: Rais Magufuli asema dereva aliyepaswa kuendesha MV Nyerere hakuwepo

Sasa imebainika kwamba nahodha wa kivuko cha MV Nyerere kilichozama Alhamisi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200 hakuwepo katika feri hiyo wakati ilipozama.

Akihutubia taifa siku ya Ijumaa jioni rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa ana habari kwamba nahodha huyo alimwachia zamu ya kuendesha chombo hicho mtu ambaye hakuwa amepata mafunzo ya kazi hiyo.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS