Home » Node

Rais Magufuli amuapisha Dkt. Asha-rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika leo tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mama Lucy Kibaki aliyefariki dunia tarehe 26 Aprili, 2016.

Mama Lucy Kibaki ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki amefariki dunia Jijini London nchini Uingereza, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Rais Dkt Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw.

Rais Magufuli Amteua Andengenye Kamishana Mkuu Zimamoto, Dkt Mmbando Mtendaji Mkuu Hospitali ya Benjamin Mkapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25 Aprili, 2016.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.

 

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS