Home » Node

Rais Jacob Zuma Htashitakiwa

Ofisi ya Mwendesha mashtaka nchini Afrika Kusini imekata rufaa hapo jana kupinga uamuzi wa mahakama kuu ulioagiza kurejeshwa kwa kesi za rushwa dhidi ya rais Jacob Zuma.

Mahakama nchini humo imedai kuondoa kwa kesi hizo kimakosa mwaka 2009 wiki chache tu kabla ya Jacob Zuma kuchaguliwa kuwa urais wa Afrika kusini.

 

Rais Dkt.Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).

Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu atoa saa 24

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ametoa masaa 24 kwa Mkuu wa Mkoa na uongozi wa jeshi la polisi na vyombo vingine  kuwasaka wauwaji hao popote walipo  na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
 
Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, ametembelea Wilaya ya Sengerema kata ya Sima baada ya usiku wa kuamkia jana kutokea mauwaji ya kinyama kwa kuuwawa  watu saba wa familia moja.
 

Rais Dilma Rousseff Atasimamishwa kazi ya urais

Bunge la Seneti Brazil limepiga kura kuamua kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo Dilma Rousseff.

Atasimamishwa kazi ya urais kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo la Seneti litakagua tuhuma zinazomkabili.

Bi Rousseff anatuhumiwa kubadili kinyume cha sheria fedha za serikali kuficha nakisi inayoongezeka ya umma kufuatia kuchaguliwa kwake tena mnamo 2014, tuhuma anazozikana.

Shutuma kuhusu shambulizi baya la anga kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Syria

Shutuma kuhusu shambulizi baya la anga kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Syria zimeongezeka leo Ijumaa wakati serikali ikikanusha kuhusika, wakati huohuo mpango tete wa kusitisha mapigano ukitekelezwa katika uwanja wa vita mjini Aleppo.

Wanawake na watoto wameripotiwa kuwa miongoni mwa raia 28 waliouawa katika mashambulizi ya Alhamisi karibu na mpaka wa Uturuki, ambayo yalijeruhi watu wengine 50.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS