Shirikisho la Wanafuzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania lampongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Kikao cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 kimeendelea tena Dodoma leo April 21 2016
Kikao cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 kimeendelea
Kikao cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 kimeendelea tena Dodoma leo April 21 2016 , shughuli nzima iliyoanza asubuhi ni maswali na majibu kwa Waziri Mkuu,
Pia baadhi ya Wizara zilihusishwa katika maswali hayo, ambapo Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara hizo walilazimika kuyatolea majibu.
Zuma amesema uchunguzi kuhusu ununuzi wa silaha haukuwa na ufisadi
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema uchunguzi kuhusu ununuzi wa silaha miaka ya tisini uliofanywa na serikali, umebaini kuwa haukuwa na visa vyovyote vya ufisadi.
Wapinzani wa serikali ya ANC kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwa Dola Bilioni 2 nukta 1 zilizotumiwa na serikali kununua silaha hizo kununua silaha hizo kutoka jeshi kutoka Mataifa ya Ulaya, zilitumiwa vibaya na kwa sababu za kisiasa.
Afisa wa juu wa jeshi nchini Burundi ameuwa akiwa juu ya pikipiki jijini Bujumbura
Afisa wa juu wa jeshi nchini Burundi
Sepp Blatter kumshawishi rais Piere Nkurunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu
Rais wa zamani wa Shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter mwaka uliopita alijaribu kuwa mpatanishi katika mzozo wa Burundi kumshawishi rais Piere Nkurunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu, lakini hakufanikiwa.
Hili nimebainika baada ya kuzinduliwa kwa kitabu kumhusu Blatter.
Blatter ameeleza katika kitabu hiki kuwa Wizara ya Mambo ya nje ya Uswizi ilimwomba kuwa msuluhishi wa mgogoro.
Huenda kati ya wahamiaji 400 na 500 wamezama Bahari
Umoja wa Mataifa unasema umetuma ujumbe wake nchini Ugiriki kuchunguza ripoti za kuzama kwa mamia ya watu waliozama katika Bahari ya Mediterranean.
Ripoti zinasema kuwa huenda kati ya wahamiaji 400 na 500 wamepoteza maisha baada ya kuzama katika Bahari hiyo.
Maelfu ya waandamanaji wapinga rais Joseph Kabila kutowania tena urais mwezi Novemba
Polisi mjini Lubumbashi Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepambana na maelfu ya waandamanaji wa upinzani wanaomtaka rais Joseph Kabila kutowania tena urais mwezi Novemba mwaka huu.

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya siku mbili.
Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya siku mbili.
Obama anatarajiwa kutumia ziara hii kuonesha ushirikiano wa nchi hiyo katika vita dhidi ya Wanajihadi.
Mzozo wa Syria na Yemen pia utajadiliwa katika ziara hiyo.











