Home » Node

Ufaransa na Misri zitaajiri kampuni mbili binafsi kusaidia katika utafutaji wa visanduku nyeusi

Ufaransa na Misri zitaajiri kampuni mbili binafsi kusaidia katika utafutaji wa visanduku nyeusi vya ndege ya Misri MS 804 iliyoanguka baharini juma lililopita wakati ikitoka Paris kwenda Cairo, Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa imesema.

Msemaji wa wizara hiyo amesema wako katika mazungumzo na kampuni mbili binafsi kwa kushirikiana na serikali ya Misri,na kuongeza kuwa lengo ni kuhamasisha vyanzo vya kuwezesha zoezi hilo kwa haraka zaidi.

Wakandarasi Wazawa kupewa kipaumbele; WALONGE NA (TAKUKURU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi kote nchini kufanya kazi kwa kutanguliza maslai ya taifa, badala ya kutaka kupata faida kubwa kupita kiasi kutoka kwenye zabuni za miradi ya ujenzi wanayopata kutoka serikalini.

Dkt. Magufuli amesema hayo 26 Mei, 2016 alipokuwa akifungua mkutano wa mashauriano wa bodi ya usajili wa wakandarasi kwa mwaka 2016 unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Maombi 52 kutoka makampuni kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini Tanzania.

MAKAMPUNI 52 YAJITOKEZA KUWEKEZA SEKTA YA UMEME

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi sasa Serikali imekwishapokea maombi 52 kutoka makampuni mbalimbali ambayo yanataka kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Mei 24, 2016) wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia.

Andre kimbuta ameruhusu maandamano

Gavana wa Kinshasa nchini DRC Andre kimbuta ameruhusu maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanyika kesho siku ya Alhamisi, Mei 26 jijini humo kufuatia mkutano na ujumbe wa jukwaa la upinzani unaotarajiwa kutolewa ikiwa ni pamoja na kupinga hukumu ya Mahakama ya Katiba ambayo inamruhusu Rais Kabila kubaki madarakani ikiwa uchaguzi wa rais utahairishwa.

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa serikali ya DRC

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzisha upya haraka iwezekanvyo mchakato wa uchaguzi na kuelezea wasiwasi wake kuhusu kunyanyaswa na kutishiwa kwa wapinzani nchini humo.

Katika mkutano wa mawaziri 28 wa mambo ya nje, Umja huo unaitaka Serikali ya Congo kupiga hatua madhubuti kuelekea uchaguzi kutokana na mvutano wa kisiasa uliopo pamoja na kusisitizia haja na umuhimu wa mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali na wadau wote kwa ajili ya makubaliano ya mpango wa wazi wa misingi ya kalenda inayoaminika na mahitaji ya kifedha.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS