Home » Node

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja

WAZIRI MKUU AONGOZA WAKAZI WA DODOMA MAZISHI YA ASKOFU ISUJA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya waumini na wakazi wa mkoa wa Dodoma katika mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Amesema kifo hicho ni pigo kwa watu wote na si kwa kanisa pekee kwa sababu walimtegemea kulisaidia Taifa kiroho na kimaendeleo.

Watu wawili wameuawa baada ya kuteketezwa moto jijini Lusaka ZAMBIA

Polisi nchini Zambia inasema watu wawili wameuawa baada ya kuteketezwa moto jijini Lusaka.

Kuanzia wiki hii, raia wa Zambia wamekuwa wakiwavamia raia wa kigeni hasa wale kutoka Rwanda kwa madai kuwa wamekuwa wakihusika na mauaji ya wazawa na kutumia sehemu za miili yao kwa sababu za kishirikina.

Ripoti zinasema raia saba wa Zambia wameuawa jijini Lusaka wiki hii na masikio, sehemu za siri na nyonyo za watu hao zikinyofolewa.

Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu (CDA).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Paskasi Muragili umeanzia tarehe 17 Februari, 2016.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe ameapishwa leo tarehe 19 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Batilda Salha Burian ambaye Mkataba wake umemalizika.

Bw. Ally Salum Hapi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Ally Salum Hapi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam.

Bw. Ally Salum Hapi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Uteuzi wa Bwana Ally Salum Hapi umeanza tarehe 18 Aprili, 2016.

 

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS