Home » Node

PPF waadhimisha siku ya Mwanake kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wazazi

Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa wazazi waliokuwa wamelazwa kweye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti katika Hospitali ya Mwananyama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo

WAZIRI MKUU Majaliwa: Rushwa barani Afrika limesababisha kupotea dola za Marekani bilioni 150 kila mwaka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema tatizo la rushwa barani Afrika limesababisha bara hilo lipoteze dola za Marekani bilioni 150 kila mwaka.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi 8, 2016) wakati akihutubia wajumbe wa mkutano wa tano wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linaloendesha vikao vyake jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulioanza Machi 6, utamalizika Machi 18, mwaka huu.

NIDA - Vitambulisho vya Taifa Vitakuwa na Saini mbili

 

 

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Utambulisho wa Taifa, Dkt. Modestius Kipilimba amesema NIDA haitafuta vitambulisha vya awali, lakini itaendelea kutoa vitambulisho vyenye saini ya mtoaji na mmiliki wa kitambulisho. 

Zoezi la utoaji wa vitambulisho ni endelevu kwa kila atakefikia miak 18, kila siku inabidi awe na utambulisho wa Taifa. Vilevile hata wahamiaji ni lazima wawe na utambulisho wanapokuwa nchini.

Majokofu chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Tumbi, hayafanyi kazi

Majokofu Maalumu ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Tumbi, hayafanyi kazi kwa muda wa siku nne sasa, hali ambayo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wafiwa wanaopeleka maiti zao katika hospitali hiyo.

Bi Eda Lemba Muhama ni Mmoja ya ndugu ambaye alifika kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kuuchukua mwili wa ndugu yake aliyefariki hivi karibuni. Anasikitishwa na hali aliyoikuta huku mwili wa ,pemdwa wake ukiwa umelazwa katika sakafu iliyotapakaa funza wanaotoka kwenye miili iliyoharibika.

Pages

Ad
Subscribe to Focus Media RSS