Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 1.65/- kwenye vyuo vya walimu
'SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 1.6/- VYUO VYA UALIMU"
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 1.65/- kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye vyuo vya walimu hapa nchini.
Alitoa kauli hiyo (Jumamosi, Februari 27, 2016), wakati akizungumza na walimu na watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.












