Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
Mgombea kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesema kuwa dunia ingekuwa mahala salama zaidi kama tu Saddam Hussein wa Iraq na Maummar Gaddafi wa Libya wangelikuwa hai.
Tajiri huyo aliyasema hayo katika mahojiano na CNN baada ya kukashifu sera za kidiplomasia za rais Barrack Obama.












